Kuanza rasmi kwa mradi wa DMDP phase 2

Kuanza rasmi kwa mradi wa DMDP phase 2

Mshobaa

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
1,714
Reaction score
677
Wakuu hivi huu mradi kuna mwenye taarifa ya utekelezaji wake?

Mwanzoni mwa mwaka huu tuliambiwa Serikali imesaini mkopo wa mabilioni kwa ajili ya kujenga miundombinu katika jiji la Dar es Salaam ambapo utekelezaji wake ungeanza mwezi june 2024 lakini hadi sasa tunaenda August bila dalili ya kuonekana greda barabarani.

Naomba kuuliza je ni lini huo mradi utaanza rasmi utekelezaji wake?
 
Wakuu hivi huu mradi kuna mwenye taarifa ya utekelezaji wake??
Mwanzoni mwa mwaka huu tuliambiwa serikali imesaini mkopo wa mabilioni kwa ajili ya kujenga miundombinu katika jiji la dar es salaam ambapo utekelezaji wake ungeanza mwezi june 2024 lakini hadi sasa tunaenda August bila dalili ya kuonekana greda barabarani. Naomba kuuliza je ni lini huo mradi utaanza rasmi utekelezaji wake???
Kwa kweli hata mimi nilikuwa najiuliza nini kinaendelea maana nilisikia mwezi wa nne mradi unaanza. Za chini chini inabidi serikali ilipe fidia kwa watakaobomolewa kupisha huu mradi, hapo ndio pana mtihani na mfadhili hatoi kitu hadi watu walipwe bila zengwe.
 
Mwanzo visingizio vilikuwa mvua kubwa zilizokuwa zinanyesha Dar es salaam. Wakasema mvua zitaposimama tu ujenzi rasmi katika maeneo yote yaliokusudiwa utaanza.

Sasa safari hii sijui visingizio vitakuwa nini. Labda watasema jua kali linasababisha mafundi wakaukiwe maji pindi wanapojenga barabara hizo nk.
 
Wakuu hivi huu mradi kuna mwenye taarifa ya utekelezaji wake?

Mwanzoni mwa mwaka huu tuliambiwa Serikali imesaini mkopo wa mabilioni kwa ajili ya kujenga miundombinu katika jiji la Dar es Salaam ambapo utekelezaji wake ungeanza mwezi june 2024 lakini hadi sasa tunaenda August bila dalili ya kuonekana greda barabarani.

Naomba kuuliza je ni lini huo mradi utaanza rasmi utekelezaji wake?
Utaenda sambamba na kampeni za uchaguzi mkuu.
 
sawa huko ni ilala na temeke ,miradi ya wilaya nyingine? Naona phase 1 walicover Kijichi na Kijitonyama/Tandalle
Hapo ndipo kwenye ugomvi wa kugombea Kati ya wabunge,madiwani na wakuu wa wilaya maana kila mmoja anatafuta Kiki kwenye eneo lake aonekane ndiye amefanya..
 
Tunategemea utekelezaji sasa baada ya Mh Mchengerwa kutia saini leo. Swali langu ni je itachukua tena muda gani wakandarasi kuingia site???
 
Back
Top Bottom