Kuanzia leo NEMC ifutwe, haitimizi majukumu yake ni wavivu wakubwa nchi hii

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,843
Reaction score
35,442
Wakuu,

Kutokana na mnakasha wa mwanajamiiforum mmoja akiilalamikia NEMC juu ya uzembe wa kutodhibiti kelele kwenye makazi ya watu na maeneo mbalimbali ya biashara napendekeza yafuatayo.

Taasisi husika ifutwe haraka maana haitimizi majukumu yake maana haiwekezani kibanda cha chupi kiwe na kipaza sauti, kibanda cha pedi kiwe na spika kubwa, kibanda cha simu kiwe na kelele asubuhi hadi jioni hii haikubaliki.

Na maeneo yenye kelele yaliyotolewa mfano ni jiji la dar es salaam limeongoza, Mwanza, Arusha, Mbeya, Tanga, Iringa, Kahama, Katoro, Ifakara, yaani wananchi wamelalamika kutokea kwa Noise Pollution ambayo haina msingi wowote kisheria.

NEMC IFUTWE NI WAZEMBE SANA NA WAVIVU.
 
Makanisa, misikiti, Bar, Nightclubs zinasababisha taharuki kwa wananchi lazima nemc ifutwe haraka ili tuanze upya
Ni sahihi alafu mkuu unakunywa zako tungi mdogo mdogo eneo tulivu mara unasikia 'PEPO LA POMBEEEEE' kutoka mtaa wa saba, wanapenda kutusema walevi wakati sisi hatuwasemi bar.

Pia usiku walokole na maombi ya kupaza, saa kumi na moja misikiti nayo yaani maisha yetu hayana utulivu kabisa.
 
Tungi inataka utulivu na mziki wa kwa mbaali sana ambao utakufanya uchezeshe mguu na kichwa taratibu kwa utulivu pale pale ulipokaa.
 
Kutokana na mnakasha wa mwanajamiiforum mmoja akiilalamikia NEMC juu ya uzembe wa kutodhibiti kelele kwenye makazi ya watu na maeneo mbali mbali ya biashara napendekeza yafuatayo.
Naona kama una hasira fulani hivi na NEMC, je uliomba ajira ukakosa?

Serikali za mitaa zina jukumu kubwa la kushughulikia mambo ya mazingira kwenye maeneo yao lakini mumenyamaza, unadhani hiyo NeMC ndiyo itakuwepo Tanzania nzima kuzuia hizo kelele?
 
Nikusahihishe sijawahi kuomba ajira kwa mtu au popote pale nchini, NEMC wanajukumu hata la kutoa waraka ambao utakua kama chain of command kuanzia wizara, mkoa, wilaya, tarafa, vijiji na mitaa, waraka huo utaelekeza hasa wenyeviti wa mazingira ambao ni wakuu wa wilaya kuunda miongozo na sheria ndogondogo ndani ya wilaya zao na hilo lifanyike kupitia mabaraza ya wawakilishi au madiwani, maana yake tayari kutakua na mlolongo wa sheria sasa kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaofanyika hapo ni kupangwa kwa faini na kutoa muda kwa watumiaji wa vipaza sauti na spika walau kufunga mfumo wa soundproof, tunachotaka ni uwajibikaji wa taasisi maana ni wazi performance yao iko chini mno, wanavizia viwandani na migodi yetu midogomidogo kuja kuchota pesa za bure,
 
Watakwambia hizo kelele sio uchafuzi wa mazingira lakini ukiwakuta huko viwandani ndio wanashikia bango na vifaa vyao maalum vya kunasa mitetemo ya sauti
 
Acha kabisa tena hata kama unakarai unachenjua dhahabu unaambiwa maji yenye mercury ni sumu hata kama umechimba karo pakuyamwaga, watakulazimisha tu ili wasitoke bure
 
Nikusahihishe sijawahi kuomba ajira kwa mtu au popote pale nchini, NEMC wanajukumu hata la kutoa waraka ambao utakua kama chain of command kuanzia wizara, mkoa, wilaya, tarafa, vijiji na mitaa, waraka huo utaelekeza hasa wenyeviti wa mazingira ambao ni wakuu wa wilaya kuunda miongozo na sheria ndogondogo ndani ya wilaya zao na hilo lifanyike kupitia mabaraza ya wawakilishi au madiwani, maana yake tayari kutakua na mlolongo wa sheria sasa kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaofanyika hapo ni kupangwa kwa faini na kutoa muda kwa watumiaji wa vipaza sauti na spika walau kufunga mfumo wa soundproof, tunachotaka ni uwajibikaji wa taasisi maana ni wazi performance yao iko chini mno, wanavizia viwandani na migodi yetu midogomidogo kuja kuchota pesa za bure,
Hili uliloandika hapa ni jukumu la Idara ya Mazingira chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais.

NEMC ni mtekelezaji wa sheria na kanuni na miongozo, Idara ya Mazingira ndiyo watengenezaji wa hizo kanuni na miongozo.
 
Nashukuru Mungu NEMC wameanza kufanyia kazi maombi ya sisi Raia wema
 
BODA BODA ZIMEFUNGWA HONI ZA TRENI na HARRIER nazo ni uchafuzi wa Mazingira. Wengine wameReset Exhaust/Eksozi zinabwatuka makelele na miripuko yaaani Afrika ni Uwanja wa fujo na Makelele tuuuu
 
Back
Top Bottom