- Source #1
- View Source #1
Taarifa kutoka TUCTA
Ndugu wafanyakazi napenda kuwataarifu kwamba kuanzia mwezi huu mishahara itakua ikitoka tarehe za mwisho wa mwezi yaani tarehe 28-30.
Lengo la kufanya hivyo ni kuondoa gap lililopo kati ya tarehe za mishahara wa sektabinafsi na sekta za Umma. Mwenyekiti wa TUCTA kasema hayo leo wakati akipongeza kuongezeka kwa asilimia ya Kikokotoo kutoka asilimia 33 mpaka 40.

- Tunachokijua
- Kumekuwa na ujumbe unazunguka katika mitandao ya kijamii ikidai TUCTA wametoa taarifa ya kubadili tarehe ya kutoa mshahara kwa Wafanyakazi wa Serikali. Tazama hapa chini:
Ujumbe unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii
JamiiCheck.com imefuatilia taarifa hii kutoka na kubaini kuwa haina ukweli.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mary Mwakapenda ameieleza JamiiCheck kuwa taarifa hiyo haina ukweli, kama kungekuwa na mabadiliko haya basi yangetolewa na Katibu Mkuu Utumishi.
Aidha, TUCTA wametoa taarifa rasmi inayokanusha uvumi huo. Tazama hapa chini:
TUCTA wakiwa wameweka chapa ya Fake kwenye ujumbe huu