Kuanzia Mwezi wa tatu nabadili ratiba za maisha(mchana naufanya usiku)

Kuanzia Mwezi wa tatu nabadili ratiba za maisha(mchana naufanya usiku)

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Habari zenu wananzengo mimi ndege John nimebarikiwa kuwa na duka dogo la mazao Na vinywaji,genge, saloon ya kiume Na Nina mpango wa kufungua duka la jeans mwezi wa pili mwishoni kwa ujumla vyote vinaweza kunipa faida ya karibia laki sita kwa Mwezi.

Bado Nina michezo ninacheza kwa hiyo kama nitakuwa Na usimamizi mzuri wa wafanyakazi waaminifu basi hela ya kula Na kuishi hainipigi chenga.kwa mfano mdada wa dukani anasimamia genge kwa siku namlipa 2000 na mwisho wa mwezi nampa 30000..kijana wa saloon jamaa yangu rasta mani yeye ananipa 5000 kila siku umeme ananunua mwenyewe na kujilipa.

Sasa changamoto nazokutana nazo Ni kukopwa Sana Na watu ninaofahamiana nao wakinikuta wananipiga mizinga Na sijui wanatumia Dawa gani kwani pamoja Na kulizwa kila siku sijifunzi ndo maana nimeamua nisiwepo ktk biashara yangu.

Sasa nataka nibadilishe ratiba niwe nalala mchana kutwa yaani kuanzia saa mbili asubuhi mpk saa mbili usiku naamka naingia gym nakula vizuri halafu nakesha nikilinda hio centre yangu huku nikisali nitakuwa nimejiepusha Na mengi sana.

Vipi huo mpango wangu Una maoni gani nitafanikiwa kweli au nishauri nifanyeje kingine Cha kuongezea kwenye Hilo wazo langu.
 
Usiogope watu waambie ukweli kioato chako hakikidhi kukopesha sana, usijitese kisa wanadamu wengi wao hawana fadhila
 
Back
Top Bottom