Kuanzisha biashara; Mambo ambayo ni ya kufahamu

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
habari za usiku
Wengi tumewahi ama kuanzisha au kufikiri kuanzisha biashara fulani.

Mara zote tunapowaza biashara kuna mambo madogo lakini ya muhimu sana ambayo huwa hatuyawazi sawa sawa ambyo hupelekea biashara zetu kufa mapema sana.

Baadhi ya mambo haya ni kama ifuatavyo:
  1. Namna unavounda wazo lako la biashara:Je wazo lako linaanza na mtaji,faida,biashara na kisha kutatua changamoto zako kisha matatizo ya jamii inaenda kwa mpangilio upi?
Nifafanue zaidi hapa:
Unapofikiria biashara wazo linaunda kwa kufikiri mtaji unaotaka au ulionao,kiasi cha faida unachotaka au kuweza kupata kisha aina ya biashara na baadaye unaangalia namna biashara yako itakvotatua changamoto zako na kisha changamoto za jamii?

Huu ndio mpangilio tunaotumia wengi na ndio maana huwa tunashindwa biashara mapema huku wale ambao wanafuata utaratibu ambao nataka niwakumbushe huwa wanafanikiwa zaidi.

Utaratibu ninaozungumzia ni kama ifuatavyo:

Kwanza kabisa kama mjasiriamali yakupasa kuangalia kwa makini changamoto zinazokabili jamii inayokuzunguka.Changamoto ziko nyingi sana na mara nyingi kila changamoto huwa ni fursa.Changamoto inaweza kuwa ukosefu wa huduma fulani,upungufu wa huduma fulani,au hata swala tu la ubora.Lazima unapotaka kuanzisha biashara uangalia changamoto zinazokabili jamii inayokuzunguka.Mara nyingi unatakiwa ufahamu kuwa zilie kero zinazokukabili ndio pia zinawakabili watu wengine wanaokuzunguka hivo ukifahamu kero hizi basi ni rahisi wewe kuunda biashara kwa kutafuta suluhu ya tatizo linalowakabili

Pili zungumza na wadau,usiogope kuzungumza kwa hofu ya kuibiwa wazo lako bado wewe kama muanzilishi wa wazo una nguvu katika wazo lako.Iwapo unaweza kuweka wazo lako katika maandishi liweke au hata tafuta mtaalamu akuwekee wazo hili katika maandishi na unapompa mtu nakala hakikisha anasaini mkaba wa usiri.Unapozungumza na wadau wafuate kulingana na nafasi yao katika wazo lako.Wengine waweza kuwa wateja wako,watoa huduma(Suppliers),wawekezaji,taasisi za fedha au hata wanaweza kuwa washindani wako kibiashara.Zungumza nao na uwasikilize kwa makini bila papara.

Baada ya kuzungumza na wadau weka scope ya kazi.Hii inakusaidia kutambua nini kinapaswa kufanywa na nani,nini ambacho huwezi kufanya au unapaswa kujifunza.Angalia pia ghara za uanzishaji na uendeshaji kwa angalau miaka mitatu ya mwanzo.Baada ya kuweka taarifa zako sawa kwa mujibu wa wazo lako rudi tena kwa wadau kwa mara ya pili huku ukiwa umefanyia maboresha kwa mujibu wa maoni yao.Ni muhimu sana ukawaambia kuwa umefanyia kazi maon yao na umeyachukua na kuyaweka na kuwaambia kuwa unawashukuru ili waweze kukupa madini zaidi.

Baada ya kukamilisha hatua hii ya utakuwa na wazo lenye afya ambalo ama unaweza kuliuza kwa mtu au wewe mwenye unaweza kuingia katika kulitekeleza kulingana na uwezo wako.

Hatua ya muhimu ni jinsi ya kugharimia wazo lako.Kumbuka kwa sasa utakuwa tayari una wazo na mpango kazi wa miaka mitatu na tayari utakuwa na wazo la mapato na matumizi yako na hivyo basi utakachohitaji ni pesa za kuanzia.Kumbuka kuwa watu wanapesa ni wewe tu uwe unajua kuuza wazo lako.Jiulize kwanza wewe uko tayari kuwekeza kiasi gani katika biashara yako hii.Ni muhimu sana uwe tayari kuwekeza zaidi ya 50% katika biashara hasa kama wewe ndio mtekelezaji.Hata kama huna hiyo 50% unaweza kuamua kutafuta mkopo kutoka kwa ndugu,jamaa na marafiki,Usiende benki kabla ya kuuza wazo kwa ndugu jamaa na marafiki kwani huko unaweza kupata wabia watakotaka kununua ile asilimia inayobaki.

Unapohakikisha kuwa umiliki wako unafikia asilimia hamsini na iwapo tayari na angalau 25% ya kiwango unachohitaji basi nenda benki na uonani na maafisa mikopo.Waeleze kuhusu wazo lako,muda ambao unatarajia kubreak even,mpango wa mapato na matumizi namna ambavyo unataka uwe unalipa dhamana utakayoweka.I wapo mkopo unaotaka benki ni kwa ajili ya kununua fixed asset au asset yoyote basi asset hiyo ndio iwe dhamana.Kumbuka katika mabenki una uwezo wa kuzungumza nao na kukubaliana namna ambavyo unataka wa kufinance,na kwa muda gani na riba kiasi gani.Hakikisha unatafuta mkopo wenye masharti nafuu na ni muhimu ukatumia mkopo huo kwa leno ulilokusudia.

Nasisitiza kuwa hakikisha kuwa kabla ya kwenda benki kuomba mkopo basi uwe na angalau 25% ya gharama unazohitaji ili uweze kuanza shughuli mara moja.

Tuendelee kujadili zaidi juu ya mambo mengine ya muhimu
 
OK.
Nasubiri mbinu za kukuza biashara ya majeneza nipate uzoefu
Naweza kukusaidia unaweza to discount kwa mtu atakayelipia jeneza lake kabla ya kufa mfano jeneza la laki mbili analipia laki moja na kusema anatarajia kufa lini akifa ndni ya hicho kipindi basi anakula punguzo aasipokufa basi unamrudishia pesa yake,vigezo na mashati kuzingatiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…