shoka mwitu
Member
- Sep 30, 2013
- 7
- 0
Nina njozi ya kuanzisha hifadhi ya nafaka kama biashara ndogo hapa Arusha lakini sina ujuzi wa kutosha katika fani hii na sijui kama nitapata faida. Mtaji wangu ni milioni 5 tu! Nifanyaje wapendwa kwani ninapenda biashara hii tangu utoto wangu niliposoma Mwa.41:25-36 na kupata kisa hiki kizuri cha Yusufu na Farao huko Misri. Kutafakari kwangu kile alichofanya Yusufu nilipata wazo hili la kuhifadhi nafaka hivi karibuni. Mimi ni mfanyakazi mdogo katika taasisi moja ya utafiti na sina ujuzi wa kufanya biashara ila natamani sana kufanya biashara hii ili kuongeza kipato cha familia yangu huku nikihudumia jamii inayonizunguka kupitia biashara hii. Wajasiriamali tafadhalini naombeni msaada wenu muhimu!!!!!!!!