Kuanzisha distillery

Amoeba

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2009
Posts
3,288
Reaction score
791
Heshima kwenu wakuu.
Nimekuwa nikiwaza na kuwazua kuanzisha biashara mpya ya uzalishaji katika kujiongezea kipato endelevu, kuna mawazo kadhaa yapo mezani; kati ya Mengi linenivutia zaidi wazo la kuanzisha Distillery ya vinywaji vikali kutokana na Ngano, Uwele, Viazi na Malighafi nyingine ambazo kwa hakika zinapatikana kwa bei ya chee sana na kwa wingi, najua ni kazii ngumu na inahitaji muda, utaalam na pesa. Napenda kupata mawazo kutoka kwa wadau ambao kwa namna moja ama nyingine wanafahamu kitu kuhusu sekta hii. Pia ningefurahi kama kuna Engeneers waliobobea katika fani hii wakanipa mwanga kwa machinery zinazohitajika, na wapi zinapatikana. Natanguliza shukrani zangu wakuu.
 
Mkuu nadhani cha maana ni product na sio process (kama unaweza ukaweka ingredients safi, zikapimwa na zisiwe na madhara kiafya, basi you are on to a winner)

Ushauri kabla hauja-invest kwenye machinery kwanza cheki product yako hata home made wape watu wataste ili uone kama inafaa na wanaipenda na watainunua sidhani kama unahitaji vifaa vya bei kwa kuanzia)

Anyway angalia hii link kwa kuanzisha same think (requirements kwa marekani) am sure process zitakuwa sawa

How to Become a Micro-distiller of Alcohol | eHow.com
 
Ni wazo zuri sana. Hapa A - town, kuna jamaa wanaitwa Mega Trade wao wanatengeneza spirits na brand yao kubwa ni Kiroba original gin. Kwa kweli walianza kwa kudharauliwa lakini sasa ni matajiri wakubwa.
Tunao mfano wa jamaa wa Banana Investment watengenezaji wa banana wine ambao walianza kama mchezo na sasa ni matajiri.
 
Reactions: LAT

Nashukuru sana mkuu kwa maoni yako, kabla sijaenda commercial nafanyakazi kwenye karatasi kwanza nione gharama za mradi wenyewe then niingie sokoni kidogokidogo, ASante!
 
Ni kweli mkuu au kwa kuanzia unaweza ukaanza na products ambazo zinajulikana (hizi pombe za kienyeji) mfano mbege, rubisi, mnazi (kama zinaweza kuwa packaged vizuri na kupatikana mijini sehemu nzuri (mfano supermarket na hoteli kubwa kubwa) hata mimi nitanunua ila shida inakuja ukitaka mbege, rubisi au mnazi mpaka uende vichochoroni au kwenye vilabu.., kama hizi mambo zingekuwa kwenye supermarkets na mainstream.., hata hapa mimi sasa hivi ningekuwa nina glass yangu ya mbege...

Alafu kumbuka hata wanaotengeneza gongo... (ule mtambo wao ni distillery) na nina uhakika hawakutumia pesa nyingi kwa huo mtambo.., pia chombo cha kupimia alcohol sio bei mbaya kabisa.. (my point being ukiwa na product huitaji kuwa na vifaa vyako unaweza kwenda hata kwa breweries / chibuku au wale jamaa wa Arusha na ukaingia nao terms za wenyewe kutumia vifaa vyao alafu mnagawana mapato ni pombe inakuwa na brand yako
 
Huo mradi wako inabidi usubiri kidogo bana, watanzania hatuhitaji pombe kwa sasa, zilizopo zinatosha, si unaona viongozi wetu walivyolewa? Lihurumie Taifa lako!
 

Mkuu, hao jamaa wanapatikana wapi? Naweza kupata contucts zao, nadhani itakuwa sehemu nzuri ya kujifunza mambo mawili au matatu! Asante mkuu.
 

Hahahaa, kaka wazo lako ni zuri sana, lakini mimi ningependa "kuunda" brand yangu iliyo tofauti kabisa na hzo unazosema, spirit yenye kunywewa na jinsia zote na rika zote ispokuwa watoto!
 
Hahahaa, kaka wazo lako ni zuri sana, lakini mimi ningependa "kuunda" brand yangu iliyo tofauti kabisa na hzo unazosema, spirit yenye kunywewa na jinsia zote na rika zote ispokuwa watoto!
Ndio hivyo mkuu, ila mimi siongelei brand naongelea process.., yaani apart from ingredients wine zote zinatengenezwa sawa, na apart from ingredients spirits zote zinatengenezwa sawa (yaani konyagi, viroba, gongo n.k.) hivyo basi unaweza kutumia mitambo ya gongo kutengeneza brand yako, ingawa hii ukaifanya bora kwa kupima kiwango cha alcohol au kuweka vionjo tofauti (ingredients) ndio maana nikasema kwa kuanzia unaweza kutengeneza chupa chache as sample kwa kutumia mtambo wa gongo wa mtu huko mitaani..

Tena kama unapenda brandy (ambayo hii huwa ni tamu zaidi) unaweza kutengeneza wine alafu ukaifanyia distallation cheki hapo chini ambavyo unaweza kutengeneza brandy hata weekend moja ukiwa jikoni kwako bila kutumia pesa nyingi kununua vifaa

How to Make Home Made Brandy | eHow.com
 
Fikiria kutengeneza Beer ,kwa bei poa ,nikimaanisha below 1000 retail price.
China mtambo wa kuunda beer ni around dola 50 elfu.pia ipo midogo ya hapo.
 
Reactions: LAT
wazo lako ni zuri sana kwa dunia ya sasa mitambo inapatikana na kama walivyosema wenzangu utengenezaji wa gongo ndio distiling process.kama uko very intersted ni pm kwa ushirikiano zaidi
 
nimeipenda hiyo ya bia ya bei nafuuu. Kenya kuna jamaa na mkewe wameanzisha KEROCHE BREWERY wakaja na brand ya bia zao ikiwamo KEROCHE LAGER imekamata soko ile mbaya...jamaa ndio chairman wa kamapuni na mama ni CEO....they are among richest kenyans now....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…