SoC02 Kuanzisha maabara ya Kiafrika

Stories of Change - 2022 Competition

Tibaiwa

Member
Joined
Sep 8, 2021
Posts
51
Reaction score
38
MAABARA YA AFRIKA.

Maabara ni chumba au jengo maalum ambalo linawezesha ufanyikaji wa majaribio ya kisayansi na tafiti mbalimbali za kisayansi.

Bara la Afrika limepitia vipindi vigumu vya mabadiliko ya kitabia ya nchi yanayosababisha kuibuka kwa magonjwa mbalimbali yanayosababisha vifo vya watu wengi sana, magonjwa haya ayasababishi tu kupunguza ongezeko la watu kupitia vifo bali magonjwa haya yamesababisha mateso ya mwili, akili na kuacha wimbi kubwa la wategemezi.

Mfano wa magonjwa maarufu ambayo yamesababisha na yanaendelea kusababisha maelfu ya vifo ni pamoja na;

Gonjwa la ukimwi, Ebola Uviko 19 pamoja na magonjwa mengine mengi.

Tangu Ugonjwa wa ukimwi ugundulike nchini mwaka, mpaka sasa imepita miaka, lakini tiba ya kuliponyesha gonjwa hili bado haijapatikana bali tu hile ya kupunguza nguvu ya virusi vya Ukimwi na kurefusha maisha na hata hivyo dawa hizi hazipatikani wala kuzalishwa ndani ya bara la Afrika bali zimetoka nje tunapoamini kuwa wao wameisha endelea. “hii ni dalili ya wazi kuwa tunapuuzia au hatujishugulushi katika kutafuta suruhu ndani ya bara letu”.

Sababu ya kusema hivi ni kuwa kupitia dawa ambazo zimeisha onyesha dalili ya kufubaza nguvu hizi zingelikuwa zimeisha chunguzwa ndani ya maabara hii na kujua zimetengenezwa na nini au hiyo dawa ya kufubaza inaweza kupatikana kwenye mimea ipi ili iongezwe nguvu ya kutibu kabisa kuliko kufubaza nguvu za ugonjwa. Hii si kwa upande tu wa ugonjwa wa ukimwi hata kwa Ebola na Uviko-19.


NINI KIFANYIKE.

Tunahitaji Maabara ya kiafrika “Laboratory For Africa Research” (LFAR).
Lengo kuu la Maabara hii ni “kuweka nguvu ya pamoja kama bara” katika kushughulikia masuala yanayo gusia Afya za raia kwani kila gonjwa linalotokea duniani vyombo vyote vya kidunia vinaiangazia Afrika kama bara litakalo athirika zaidi bila hata ya ushahidi wa kichunguzi.

Sisemi kwamba hatuna maabara za kushugulikia magonjwa ya milipuko pale yanapotokea nchini, tunayo lakini nguvu kazi yake ni ndogo kupitia wataalamu waliopo na vitendea kazi vilivyopo. Mfano hapa Tanzania tuna

Maabara hii ya bara la Afrika ikianzishwa itaunganisha nguvu ya pamoja kutoka kila nchi kwa kushughulikia tatizo la kiafya litakalokuwa linajitokeza huku taasisi za kushughulikia masuala hayo kwenye nchi husika zikipeleka sampli za ugonjwa, janga la kiafya linaloikumba pamoja na dawa zinazokuwa zimependekezwa kwenye nchi ili maabara hii kupitia wabobezi itakao kuwa nao pamoja na vifaa bora vya kisayansi wakae pamoja kwa kukusanya dawa zitakazotokana na mapendekezo ya nchi zingine kupitia tafiti ndogo naza dharura ili itengenezwe dawa moja itakayokuwa bora zaidi kwa ajili ya kutibu gonjwa litakalokuwa limejitokeza baada ya utafiti wa kina kwani zile dawa za kupunguza nguvu ya ugonjwa unaojitokeza zinaweza kutoa mwanga wa kutafuta suruhu ya kudumu.

Hii italeta suala la urasmi na kuondoa mkanganyiko wa kutumia dawa nyingi za majaribio zinazoweza kuwa hatari kwa afya ya mwanadamu vilevile itaondoa hali ya kudogodisha tiba zinazotoka Afrika kwani visa vya kovidi -19 vimetupa funzo pale hata shirika la afya duniani WHO lilipoonyesha mashaka juu ya dawa zilizokuwa zikipendekezwa na Afrika kama hile ya nchini Magadaska na nchi nyingine huku wakiendelea kusema mawimbi makubwa yataikumba Afrika, Maabara hii itakuwa na nguvu ya kiteknolojia na kifedha itakayoipata kutoka kwa wanachama wake.

Maabara hii itasaidia kuandaa wataalamu wa afya kutoka kila pembe ya nchi ndani ya Afrika kwa kuwaandaa mapema na kuwapatia mafunzo yatakayoendana na mahitaji yatakayo kuwepo.

Bado ninayoimani kuwa miti ndiyo chimbuko kuu la dawa zinazopatikana duniani hivyo maabara hii itakuwa mstari wa mbele kuitafiti miti iliyokuwa inatumika kama dawa tangu zamani kwa kuichunguza kupitia tafiti ili kuvuna dawa zitakazokuwa zinatumika kama tiba kwa kuziondoa sumu isiyohitajika na hapa itasaidia kwenye uhifadhi wa hiyo miti pamoja na hile itakayoonyesha dalili za kuwa na uwezekano wa kutoa tiba mbalimbali na kuziboresha hizo tiba kwa kuzitoa kwenye uenyeji na kuzipeleka kwenye tiba za kisasa.

Nguvu hii ya pamoja itakayotokana Maabara ya (LFAR) italeta matokeo ya udhiti wa pamoja kwa magonjwa yatakayokuwa yanaibuka kwenye nchi kuliko mzingo huu kuilemea nchi moja inayokumbwa na gonjwa linaloibuka kwani kupitia maambukizi yanayoenea hayajali tu nchi moja ambayo ugonjwa umeibukia.

Mfano ugonjwa wa Ebola unaonekana kuzitesa nchi za Afrika Magharibi na kuzifanya kanda zingine zione kuwa hazina haja ya kudili nao lakini ukianza kusambaa kwenye kanda zingine ndipo itakapoonekana “uhitaji wa nguvu hii ya pamoja “. Ninayoimani kubwa kama Afrika tungekuwa na Maabara hii tungelikuwa tumeisha pata suruhu ya ugonjwa huu unaowasumbua wenzetu na mengine mengi yanayotusumbua sisi au hata kuyadhibiti katika kuenea kwa kasi kubwa baada ya dawa za kuyapunguza nguvu kupatikana.

Kupitia mahabara hii tunaweza kuwa na shirika la Afya Afrika litakalokuwa na nguvu iwe kwa kushirikiana na lile la dunia WHO au linalosimama peke yake, shirika hili la Afrika liwe msimamizi mkuu wa maabara hii huku wanachama wake wakiwa ni taasisi zinazoshughulikia na magonjwa ya mlipuko kutoka kila nchi ya Afrika. Huku wabobezi wa Afya na tiba wakiwa wasimamizi wake ndani ya Afrika.

“Maabara hii iwe pia na uwezo wa kutambua chimbuko la vimerea vya magonjwa ili kuondoa migogoro tunayoiona juu ya chanzo cha magogonjwa yanayolipuka yaani iwe na uwezo wa kutambua kama virusi vinavyotokea na kuenea vijulikane wazi wazi kama nivya kutengenezwa kwenye maabara au vinatokana tu na mabadiliko ya tabia ya nchi yaani ni asili iliyopo bila mkono wa mtu kuhusika kupitia maabara”.

“Ushahidi wa kimaabara utasaidia kuwabaini watengenezaji wa virusi na kuwawajibisha kisheria”Ninayoimani kubwa kupitia maabara hii kutapunguza utegemezi mkubwa wa misaada ya kiafya kutoka nje ya Afrika na itazalisha wabobezi watakaokuja kuwa msaada mkubwa hapo baadae kwa bara la Afrika.
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…