Uwe na katiba nakala 8 iliyopitishwa na wanachama. Cv za viongozi zilizobandikwa picha upande wa kulia. Barua ya kuomba Usajili kwa katibu tawala wilaya, barua ya utambulisho toka mtaani ilipo NGO pamoja na ya mtendaji wa kata, muhtasari wa kikao ulipoitisha katiba pamoja na saini zao, saini za waanzlishi wa NGO. Lazima uwe na ofisi na physical address. Nenda kwa afisa tarafa wa eneo husika, atakukagua na kukupa maelezo mengine.