Kuanzisha thread JF ujipange

Shida na raha

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2014
Posts
3,773
Reaction score
3,471
Habari za majukumu wakuu wenzangu na wadogo zangu pia.

Sababu ya kusema hivi ni kwamba nimeangalia wanajamvi kwenye huu mtandao ni wengi mno ila wanao anzisha mada ni wachache sana.

Kwanza:
Mimi kwa mawazo yangu nahisi wengi wao wakiona mtu kaanzisha mada jinsi anavopambana na watu humu itakua wanahofia kuja kukutana na dhoruba kama hizo.

Pili:
Kujiamini na kupata ujasiri wa kuweka thread yataka moyo na ujasiri, sasa pengine mtu hajiamini.

Tatu:
Mtu hapendi kuja kulumbana na watu maana pengine ukimtizama tu analia sasa anaogopa kuja kuzidisha machozi hapa.

Mengine ni masuala ya mtu binafsi anajua mwenyewe kwanini hata kama ana shida ya kutaka kujua kitu kupitia hapa hawezi kuja kuweka thread yake.
Mwisho niwapongeze wale wote ambao wakiweka thread hapa wanakutana na masahibu makubwa lakini wanavumilia vishindo.
 
njoo jukwaa letu pendwa la wakubwa hakuna ubaguzi huko yoyote anatupia tu ile kitu roho inapenda
 
Watu wanaona ufahari kupata likes na comment nyingii wakati tumboni njaa inauma
 
JF WANAZINGUA KTK KUAMZISHA THREAD MPYA.
 
njoo jukwaa letu pendwa la wakubwa hakuna ubaguzi huko yoyote anatupia tu ile kitu roho inapenda
Hili jukwaa lipo mitaa ya wali mkuu....[emoji53] [emoji53] [emoji53]
 
Nini kifanyike...leo fb kunasemaje btw??
 
Nini kifanyike...leo fb kunasemaje btw??
Kule sasa hivi nimekuwa na magroup mawili, moja linanikubali moja halinikubali.

Sababu ambayo group halinikubali:

Naweza kupost picha za hela tsh au dola basi baadhi roho zinawauma kuona zile pesa maana utakuta kwa wakati huo kuna mtu vyuma vimemkaza sana. Aidha anadaiwa au ana shida japo elfu 10 hajui atoe wapi.

Kundi linalonikubali ni kwamba mimi silazi damu, ukija kichwa kichwa kwenye post yangu, utaondoka ukijiuliza hivi ndo yule ambae namuona mstaarabu? Kumbe umekuja kutafuta sifa ili watu wakuone wa maana lakini nakupa makavu.

Wengine sasa hawa like, wala kukoment maana niliwapiga mabomu ya motor hawatosahau.
Ila pia nina marafiki wengi akina dada nikiweka picha tu lazima like nyingi ziwe za kwao mpaka kuna aliekuwa dem wangu kanichunia sababu:
Kuna wadada watano wanawahi seat sasa kile kitendo kilimkera na kunambia ni madem zangu, nilibaki mdomo wazi.

Kwa ufupi nina changamoto sana njoo ujionee mwenyewe.
 
Wote tukianzisha nyuzi humu nchi haitakalika hii,wengine tunachungulia,tukiona kuna jipya tunaconcentrate,tukiona ni yale yale tunasepa,tukiwa na jipya na sisi pia tunaliwasilishwa kwa wajumbe humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…