Kuanzishwa darasa la kujifunza kisukuma Marekani (US)

Kuanzishwa darasa la kujifunza kisukuma Marekani (US)

Uliza_Bei

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2011
Posts
3,216
Reaction score
990
Kuna jamaa yangu (research scientist) alikuja hapa nchini akafanya kazi Mikoa ya Mwanza na Shinyanga. katika mambo aliyojifunza Tanzania ilikuwa ni pamoja na lugha ya kibantu ijulikanayo kama kisukuma. huyu jamaa kwasasa yuko California na anataka kuanzisha darasa la kufundisha watu kisukuma hapo Marekani (US). Amenifurahisha sana, nimejitolea kumpa biblia aliyoiacha babu yangu (kwa lugha ya kisukuma) na kitabu cha tenzi za rohoni (kwa lugha ya kisukuma). Sikuwa na vitabu vya kisukuma vya hadithi na mengineyo. Kama unapenda kushirikiana na huyo jamaa kwa kuboresha darasa lake la kisukuma karibu.

Jihabarishe hapa kama ulikuwa huji kuwa hii nayo ni lugha kubwa kuliko hata kiswahili kwa maana ya kuongelewa na watu:
Kisukuma ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wasukuma. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kisukuma imehesabiwa kuwa watu 5,430,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kisukuma iko katika kundi la F20. Inafanana na lugha ya Kinyamwezi:
  • Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. (Orientalia et africana gothoburgensia, no 17.) Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346-454-6
  • Guthrie, Malcolm (1948) The classification of the Bantu languages. London: Oxford University Press for the International African Institute.
  • Jump up↑ Guthrie, Malcolm (1967–71) Comparative Bantu: an introduction to the comparative linguistics and prehistory of the Bantu languages. 4 vols. Farnborough: Gregg Press.
  • Nngwabeja ba baba na ba mayu
  • Jump up
 
350px-Lugha_za_Afrika_ramani.PNGMgawanyiko wa lugha za kibantu ni kama unayoonyeshwa hapo na kisukuma kikiwa na uwakilishi mkubwa sana kwa Tanzania
 
Uliza_Bei;ngw'amisha mhola mayu?
Hahaa Sijaelewa bwana..nifundishe basi.
 
Mimi hata ukinifunza kidukuma sitaki, kwa sababu sijui nikizungumze wapi kwenye huu ulimwengu
 
"Kama unapenda kushirikiana na huyo jamaa kwa kuboresha darasa lake la kisukuma karibu."

Watani kwa kujifagiliaaa!........MUMESHINDAAA!(in kisukuma accent)
 
Obengh'we mtizo etaga mamihayo ma ng'a chilochilo henaha, kongono obise tole na maganiko ga kontogya oseba.

Maganiko genago, gakobiza manyalali getegete, nolo twale mu nzala ja se yeneye, o Seba akotowela tutizoeta mamihayo sagala.

Henaha Seba akojiwe nho banamhala noo banhiisale.

Mwabeeja geete geete.

Alii, gashinaga tolemo noobise.

Neeyo!

Mtizo haya "le Kiranga lyeta koyomba kizungu ndoho, lyetagi gete litamanile koyomba sha kokaya getegete".

Nene nateho kwenuko.

Okwiza na sha kokaya nalemo, olo obize kohaya ole nswahili, nalemo, olo obize nolo na kiingereza, nalemo.

Onzukulu wo chalo akamana pye nzela.
 
Hata mimi sikujua hilo! lakini ni kwa kuzungumzwa tu siyo vinginevyo tena TANZANIA TU

Kwa hiyo kisukuma ndo kinatumika hadi wapi sasa kama si tanzania tu tena na watu wachache.. kwa kua ni lugha ya kibantu doesn't make t the most spoken language, kwani kiswahili hakijatokana na kibantu?? kulinganisha kiswahili ni kisukuma ni sawa na kulinganisha tanzania na US kwa uchumi.... nenda nchi za watu uliza lugha wanayotumia afrika watakwambia kiswahili, hata hawajui kama waafrika tuna lugha tofauti kila kona... na wakenya wote wanajua kiswahili weka hilo akilini, wacongo wanaoongea nao wapo, rwanda, burundi.. na kinafundishwa hadi vyuoni china, korea, japan, usa, huko hawajasikia neno kisukuma
 
Back
Top Bottom