Kuanzishwa kwa "Madarasa janja" kwa mujibu wa Waziri wa Elimu, Prof. Mkenda

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Nikiwa naangalia taarifa ya habari, nimesikia waziri akisema wanataka kuanzisha madarasa janja akimaanisha "smart classes"

Nawaheshimu sana watu hawa wanaoitwa Prof. kwani wengi wao wamepita njia ngumu kufika walipofika.Hata hivyo hoja yangu sio kuanzishwa kwa "madarasa janja" hoja yangu ni tafsiri ya neno "smart" kwa lugha ya kiswahili kuwa ni "janja"

Je ni kweli hiyo ndiyo tafsiri?Ina maana Prof na wataalamu wote wizarani walishindwa kujua neno halisi linaloweza kuwa sawa na smart?

Tafsiri ya neno hilo ilianzishwa na Masoud Kipanya akijaribu kutafsiri neno "smart phone" akiita "simu janja".Kama tu mzaha vile kila aliyesikia akajua hiyo ndiyo tafsiri rasmi. Sasa watu wa kawaida ikawa ndiyo neno lao kuitambulisha smart phone. Shida inakuja pale wasomi nao, tena katika wizara nyeti,kuvutiwa na neno janja ( clever) kuwa lina maana ya smart bila kuchakata kidogo kupata neno halisi.

Nawapenda wakenya kwa kuwa kiswahili wanakijali na wao wanaita smart phone kama " simu tanashati"
Badala ya kuita madarasa janja ni bora wangeita darasa tanashati.Neno janja ni kama linaashiria utapeli,uswahili Swahili na mtu kutaka kulipua lipua kazi mradi awe wa kwanza kumaliza.

Mtu akikwambia acha ujanja ujanja ni kama anakwambia acha ubabaishaji.

Mimi sio nguli wala kamange wa lugha lakini nakereka kuona hatuchakati mambo na wakenya wanaoneka wako mbele yetu kwa mambo mengi.
 
Hata miye nilishtuka kusoma kichwa cha habari hii kabla ya kuzama ndani kwani nilielewa ni madarasa ya kitapeli. Yaitwe "Madarasa tanashati" au "Madarasa nadhifu"
 
Smart phone kuiita simu tanashati hiyo ni tafsiri sisisi. Ni bora sana kuitwa simu janja.
 
Iko hivi: Lugha ni mali ya jamii na siyo ya Profesa Mkenda wala BAKITA. Jamii ikiamua msamiati fulani utumike na ukakubalika basi utatumika tu. Ndiyo maana BAKITA wana mamisamiati yao mengi tu lakini wamebaki nayo huko kwao na mitaani hayasikiki. Eti keyboard iitwe baobonye, liquid ni ugiligili...kha!

Darasa janja ni sawa maana jamii inaweza kupanua zaidi wigo wa matumizi ya hilo neno na likakubalika tu. Hata darasa tanashati ni yale yale maana utanashati kimsingi ni unadhifu wa mwili. Sasa sijui hii inakamata vipi dhana ya smart class.

Mjanja - mweledi, mwenye akili, mwerevu, laghai (cunning) n.k.

Darasa janja ✅️✅️✅️👏👏👏
 
Mimi nadhani lugha inawaze kujisinania yenyewe bila kutafuta tafsiri ya neno. Mfano hapo tumeona wataalamu wa Kenya wametafsiri neno smart kama tanashat hivyo kupata neno simu tanashati na huku Tz nao wametafsiri neno smart kama janja wakapata neno simu janja, ila mimi kama mtu wa kawaida na siyo mtaalamu wa lugha ya kiswahili hizi smartphone huwa naziita simu MPANGUSO, binafsi huwa naona hii inasound vizuri. Kuhusu smart class hii mimi ningeita darasa VIPANGA au VIPAJI hii ingesound vizuri kuliko kutafsiri neno moja moja.
 
Nikiwa naangalia taarifa ya habari, nimesikia waziri akisema wanataka kuanzisha madarasa janja akimaanisha "smart classes"

Nawaheshimu sana watu hawa wanaoitwa Prof. kwani wengi wao wamepita njia ngumu kufika walipofika.Hata hivyo hoja yangu sio kuanzishwa kwa "madarasa janja" hoja yangu ni tafsiri ya neno "smart" kwa lugha ya kiswahili kuwa ni "janja"

Je ni kweli hiyo ndiyo tafsiri?Ina maana Prof na wataalamu wote wizarani walishindwa kujua neno halisi linaloweza kuwa sawa na smart?

Tafsiri ya neno hilo ilianzishwa na Masoud Kipanya akijaribu kutafsiri neno "smart phone" akiita "simu janja".Kama tu mzaha vile kila aliyesikia akajua hiyo ndiyo tafsiri rasmi. Sasa watu wa kawaida ikawa ndiyo neno lao kuitambulisha smart phone. Shida inakuja pale wasomi nao, tena katika wizara nyeti,kuvutiwa na neno janja ( clever) kuwa lina maana ya smart bila kuchakata kidogo kupata neno halisi.

Nawapenda wakenya kwa kuwa kiswahili wanakijali na wao wanaita smart phone kama " simu tanashati"
Badala ya kuita madarasa janja ni bora wangeita darasa tanashati.Neno janja ni kama linaashiria utapeli,uswahili Swahili na mtu kutaka kulipua lipua kazi mradi awe wa kwanza kumaliza.

Mtu akikwambia acha ujanja ujanja ni kama anakwambia acha ubabaishaji.

Mimi sio nguli wala kamange wa lugha lakini nakereka kuona hatuchakati mambo na wakenya wanaoneka wako mbele yetu kwa mambo mengi.
Naunga mkono hoja.
 
Tujitafakari tulipokosea tujisahihishe
Tusifuate mkumbo tufuate njia sahihi.
 
Neno smart litafsiriwe kama 'kamilifu'. Hivyo smart class ni darasa kamilifu
 
Back
Top Bottom