Kuanzishwa kwa Redio (Rungoya)

Kuanzishwa kwa Redio (Rungoya)

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Historia ya kuanzishwa kwa Redio

Mwaka 1886 Mjerumani Heinrich Hertz alitambua mawimbi ya sumaku umeme. Wataalamu na muhandisi mbalimbali walifanya majaribio katika miaka iliyofuata kutumia mawimbi haya kwa mawasiliano, kati yao Mwitalia Guglielmo Marconi, Mmarekani Nikola Tesla na Mrusi Alexander Popov. Kila mmoja ametajwa kama "mtu wa kwanza aliyegundua rungoya".

Kituo cha kwanza cha rungoya kilianzishwa na Mholanzi Hanso Schotanus à Steringa Idzerda tarehe 6 Novemba 1919 aliposambaza muziki kutoka nyumba yake. Kituo cha kwanza cha kibiashara kilianza kazi mwaka 1920 Marekani mjini Pittsburgh.

Katika miaka iliyofuata redio ilisambaa kote duniani. Ni njia muhimu ya kusambaza habari pamoja na utamaduni, hasa muziki.

Matumizi ya redio
Hapo zamani, redio zilitumika na mabaharia kwa kutuma jumbe toka chombo majini hadi nchi kavu kwa kutumia kodi za Morsi (Morse code). Wakati chombo kilichojulikana kama Titanic kilikuwa kinazama mwaka 1912, jumbe zilitumwa kutoka kwa mabaharia waliokuwa kwenye chombo hicho kwa vyombo vilivyokuwa karibu.

Wanajeshi pia walitumia redio kutuma jumbe na kuwasiliana na makao yao makuu.

Leo, redio hutumika kwa mawasiliano, matangazo na muziki. Kabla ya uvumbuzi wa televisheni, redio zilitumika kwa uigizaji na vichekesho. Redio za leo zinatumia wavu za dijitali na huweza kushika wavu kwa urahisi zaidi.

Pia kuna redio za kushikwa kwa mikono.
 
Back
Top Bottom