Aspergillus
Member
- Jun 19, 2023
- 6
- 5
Utangulizi
Bunge mkononi litakuwa ni bunge/mkutano utakaompa nafasi kila mwananchi kuwa mbunge. Bunge hili litakuwa kwa njia ya mtandao, na mshiriki ataweza kushiriki kupitia sim janja ya mkononi. Mtu aliye tayari atajisajiri katika mtandao wa bunge utakaoanzishwa, na maombi yatatumwa selikalini ili kutambuliwa kwa Tanzania bunge mkononi na kuweza kujadili hoja za mhimu kabla hazijafikishwa kwenye bunge kuu.
Maelezo kiundani, na tatizo lililokuwepo
Bunge ni sehemu maalumu ambapo wawakilishi wa wananchi hukutana ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi kiusalama na kimaendeleo. Wawakirishi hao huchaguliwa na wananchi wenyewe kwa mujibu wa katiba, hivyo basi mtu aliechaguliwa huwasilisha hoja kwa niaba ya mamia ya maelfu ya wanachi waliomchagua.
Sababu kubwa ya kuchagua wawakilishi ni kwamba, ni vigumu sana kwa wananchi wote kukusanyika sehemu moja na kutoa maoni yao, hivyo basi inawalazimu wananchi kuchagua wawakilishi. Kama ingewezekana wananchi wa nchi nzima kukaa kikao pamoja basi kusingekuwa na haja ya uwepo wa bunge. Kutokana na wingi wa watu haiwezekani raia kukaa sehemu moja na kufanya kikao pamoja, hivyo basi njia pekee sahihi ya kushiriki mkutano wa taifa zima ni kupitia kuchagua wawakilishi kwa njia ya kupiga kura.
Kulingana na senya ya watu na makazi ya mwaka 2022, Tanzania ina jumla ya watu milioni 60 ambao huwakilishwa na wabunge 393 kiujumla. Hivyo basi kwa wastani kila mbunge mmoja huwakilisha wananchi laki moja na nusu.
Kwa miaka hii wananchi hawafurahii na kuwakirishwa na mtu meingine, hiyo husababisha vijana wengi kususia uchaguzi kutokana na kupoteza imani na wawakilishi wao wanaowachagua awamu zote. Hii imetokana na kwamba wawakilishi wengi wanaochaguliwa hutafuta wadhiwa wa ubunge kwa masirahi yao binafsi, au masirahi ya vyama vyao vya siasa hivyo basi kuwafanya kujadili hoja huku wakiwa na ushabiki wa vyama vyao na masirahi yao. Lakini pia wawakirishi wengine hawaoni haja ya kusimama na kutetea wananchi wake, na hubaki kimya kwa miaka yote wakati wa vikao vya bunge.
Hali hii huwakasirisha vijana na kuona kuwa taifa linapoteza mwelekeo kwa sababu hawana namna ya kutoa maoni wao wenyewe na kusikilizwa, huku upande wa pili wawakirishi wao wakiwasilisha maoni tofauti na matarajio ya wananchi wasio wabunge. Hivyo bas vijana wengi imewafanya wavunjike moyo kujihusisha na siasa na badala yake wamejikita zaidi na maisha yao binafsi ili kuweza kunusuru familia zao katika mahitajinya kibinaadam, kuliko kuendelea kufuatilia siasa.
Utatuzi wa tatizo lililowasilishwa
Kupitia jukwaa napendekeza kuanzishwa kwa TANZANIA BUNGE MKONONI inayotambuliwa na selikali. Hili litakuwa ni bunge kwa njia ya mtandao, ambapo kila mmwananchi atakuwa huru kujisajili kwa namba na NIDA na kuwa huru kutoa maoni kwa njia ya Video, Audio au maandishi.
Selikali itaombwa kuhalalisha bunge hili liwe sehemu ya bunge kuu la selikali, ili maada mbalimbali za maendeleo na usalamna zijadiliwe na wananchi wote kupitia TANZANIA BUNGE MKONONI baada ya hapo itawasilishwa bunge kuu kujadiliwa zaidi, huku wakichaguliwa wawakilishi maalumu wa TANZANIA BUNGE MKONONI (TBM) Kwenda kuwasilisha hoja zilizojadiliwa kupitia TBM.
Bila kutukana wala kumkashifu kiongozi wa selikali, wala kumkashifu raia yoyote, mwananchi mshiriki wa TANZANIA MKONONI BUNGE atatoa maoni yake, na maoni yake yatasambazwa tovuti mbalimbali.
Kila wizara itakuwa na sehemu yake, katika TBM na selikali itaombwa kuweka sheria ili wizara husika ziwe zina shughulikia maoni ya (wananchi wabunge) kila baada ya kipindi cha muda flani.
Endapo mtoa maoni (mshiriki wa TANZANIA BUNGE MKONONI) Atavunja sheria kupitia wakati wa utoaji wa maoni, atawajibishwa kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kuzuiliwa kwa muda utoaji wa maoni kupitia TANZANIA BUNGE MKONONI. Hivyo basi kila mhsiriki atazingatia nidhamu pamoja na kufuata sheria zilizowekwa za nchi.
Katika sehemu ya mtoa maoni, mtoa maoni ataonesha yeye ni wa chama gani, aidha kama hana chama ataonesha pia kwamba hafungamani kabisa na chama chochote.
Sanjari na hayo katika online bunge hiyo kutakuwa na sehemu ya maktaba, ambapo kutakuwa na vitabu vya kidijitali vya kuelimisha wananchi.
Vitabu hivyo vitajumuisha katiba ya wananchi, vitabu vya uraia kufundisha wananchi mifumo ya utawala, alama za barabarani, haki sawa, elimu ya rushwa, pamoja na historia ya Tanzania. Mtu ataingia sehemu ya maktaba kwa hiari yake ili asome na kuongeza uelewa juu ya nchi yetu Tanzania. Lakini pia kama mtoa maoni atatoa maoni na kuashiria kuna kitu fulani bado hajakifahamu katika katiba au utawala, basi wadau watamwelezea vizuri ikiwa ni pamoja na kumuonesha andiko husika ili asome na kuelimika.
Aidha pia katika sehemu ya mtoa maoni kutakuwa na sehemu ya wadhifa wake, ili kuonesha mafanikio yake katika siasa au tasnia yake nyingine anayonihusisha nayo.
Sanjari na hayo, sehemu ya mtoa maoni kutakuwa na sehemu ya kutoa taarifa za siri, ambazo anahofia endapo zitamuacha katika hali ya wasiwasi kiusalama kama zikiweza kusomwa na kila mtu. Taarifa hizi ni kama taarifa za uwepo wa ugaidi, au wahamiaji haramu, wanaoshirikiana na wazawa kuingia nchini na kuweza kudhoofisha usalama wa raia na mali zao, kufichua viongozi wala rushwa sehemu za barabarani, hospitalini, maofisini na na sehemu nyingine kwenye huduma za kiselikali. Aidha pia mtoa maoni ataweza kutoa taarifa za juu ya wahadhiri vyuoni wanaoomba rushwa za ngono kwa wanafunzi wao. Taarifa nyingine za siri zitakazowasilishwa ni pamoja na kufichua wazazi wanaowaoza watoto wao ingali bado ni watoto na wengine wanaoozwa wakiwa bado wapo masomoni. Taarifa hizi zitaweza kuonwa na mamlaka husika tu, hivyo bai watoa taarifa watakuwa na uhakika wa usalama.
Mchakato wankuchagua wawakilishi wa TANZANIA BUNGE MKONONI utafanyika kwa kuangalia ni maoni gani yamependwa na raia wengi, kwa hiyo basi wahusika wa maoni hayo wataitwa bungeni kuweza kuelezea kimapana zaidi juu ya maoni yao.
Hitimisho
Bunge hili litafanya wananchi walio wengi kuweza kufikisha maoni yao kiufasaha, kupunguza malalamiko kwa vijana juu ya siasa, kuwaelimisha wananchi juu ya katiba, elimu ya rushwa, alama za barabarani, haki za kijinsia, historia na kupanua wigo wa demokrasia kiujumla.

Upvote
6