Kuanzishwa na kuzaliwa kwa MOSSAD

Kuanzishwa na kuzaliwa kwa MOSSAD

Annuity

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2013
Posts
338
Reaction score
198
Katika kitabu cha Gideon Spies kilichowekwa na mdau mmoja wa JF nimejaribu kukisoma na nimeona nishirikishe wadau mambo kadhaa yaliyonivutia hasa katika kuundwa kwa taasisi maarufu ya kijasusi inayosemekana kuwa ina watu wenye akili na makini zaidi ulimwengu wanayoifanya Israeli indelee kudumu katikati ya msitu wa maadui Mashariki ya kati na nime rely heavily hasa katika ile Chapter ya 2. Sio kila kitu nimeandika ila yale muhimu tu na pia filamu ya The Patriots of Mossad (1994) na vyanzo vingine kwenye mitandao vimetumika.

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------​----------------

Watu kutoka miji mbalimbali ya Tel Aviv, Haifa na vijiji vya karibu ya bahari ya Galilaya ambapo wazee kwa vijana, wafanyabiashara, waalimu wa sheria za kidini na watu wa aina mbalimbali walipokuwa wamekusanyika katika hekalu la Herod the Great II katika mji wa Jerusalem katika moja ya kuta zinazoogopwa zaidi ulimwenguni, ambapo kwa wahayudi ni sehemu takatifu kwao kwa ajili ya kufanyia ibada na maombi, ukuta huo unaitwa Wailing Wall au Western Wall (The holiest shrine of the Jewish World). Katika karne nyingi zilizopita utamaduni huu umekuwa unafanywa mara kwa mara na wayahudi toka enzi za mababu zao.

Wakiwa wamevalia mavazi ya rangi nyeusi, kila mtu akiwa na kitabu chake cha maombi ambapo walikuwa wakipitia maandiko kadhaa katika vitabu vyao huku wakifanya maombi mbele ya ukuta huo, sabato hii haikuwa kama sabato nyingine zilizo zoeleka, sabato hii ilifanyika Septemba 1929 na ilikuwa ya tofauti kidogo, waalimu wao wa dini (rabbis) waliwataka watu wakusanyike kwa wingi, sio kwa sababu tu ni haki yao kufanya hivyo bali kuonesha alama ya umoja wao na uyahudi wao na kuwakumbusha waarabu waliokuwa wamewazidi kwa idadi kuwa licha ya wingi wao hawataweza kuwatawala wala kuwaonea. Na kwa miezi kadhaa nyuma jamii ya waislamu miongoni mwa waarabu walikuwa na wasi wasi na hasira juu ya kile walichokiona kupanuka na kusambaa kwa uyahudi katika eneo hilo, na wasi wasi huo ulikuja kutokana na na azimio la Balfour (Balfour Declaration) lililonesha kuwepo kwa makazi rasmi ya wahayudi katika ardhi ya Wapelestina. Waraabu hawa walikuwa na wasiwasi kuwa ardhi waliyoilima kwa kipindi kirefu inaweza kuangukia mikononi mwa wayahudi na kupoteza haki ya umiliki wake na waarabu hawakutaka hili litokee hata kidogo.

Huku Jerusalem wayahudi wakiwa katikati ya maombi mara kulisikika tafrani ambapo walianza kurushiwa mvua mawe na chupa zilizovunjwa na baada muda kadhaa pia milio ya risasi ilisikika kutoka kwa washambuliaji hao. Rapsha hiyo ilisababisha watu kuanza kukimbia hovyo na kukanyagana kila mtu akiwa katika harakati za kukimbia ili kukwepa shambulio hilo na kuokoa uhai wake, kwa bahati nzuri hakuna mtu aliyekufa ila kulikuwa na majeruhi lukuki. Usiku uleule viongozi wa Yishuv, (Yishuv ilikuwa ni jamii ya wayahudi waliokuwa wanaishi maeneo ya Palestina) walijadiliana kwa kina kuhusu maandamano waliyoyapanga na kuyafanya kwa umakini mkubwa na ujumbe waliokuwa wanataka kuutoa kuwa haukuzingatia tishio la wapalestina kuweza kuja kuwashambulia katika eneo lao hilo takatifu la kufanyia ibada.

Kutokana na kipindi hicho watu wa Israel na Palestina wote walikuwa chini ya utakuwala wa kiingereza na wote wakitegemea ulinzi kutoka kwa mtawala wao huyo, kwa tukio la Israel kushambuliwa na waarabu wa kipalestina, wayahudi waliona palikuwa hakuna haja tena ya kutegemea ulinzi huo ulioshindwa kuwalinda katika eneo lao takatifu hivyo wakaamua kuanzisha kikosi chao cha ulinzi kilichojulikana kama Hanagah neno la kiebrania linalo maanisha ulinzi, ili kuwalinda wayahudi na nchi yao sababu waliona kabisa kuwa hawataweza kuacha kufanya ibada na maombi katika sehehemu yao hiyo takatifu ya Wailing Wall.

Hanagah
kama taasisi ya ulinzi na pia ya kijajusi ilikuwa inafanya kazi ya kuhakikisha inapata taarifa zote muhimu kuhusu aina yeyote ya hatari inayoweza kufanywa na waarabu na maadui wengine katika ardhi yao, ndipo kwa umakini mkubwa walifanya kila wanaloweza na walifanikiwa kuwa recruit baadhi ya waarabu wa kipalestina wafanye kazi hiyo kwa uhai wa taifa lao. Waalimu, wanafunzi na wafanya biashara wa kiyahudi waliokuwa katika aridhi ya wapalestina na vijana wa mtaani waliokuwa wanafanya kazi ya kusafisha viatu (shoe shines) vya maofisa wakubwa wa kipalestina nao walikuwa watu potential sana katika upatakanaji wa taarifa mbalimbali kwa Hanagah.

Katika kikao kilichofanywa na David Ben-Gurion and Yitzhak Rabin (Waanzishaji wa Hanagah) katika mji wa Haifa mwaka 1942, walikubaliana kuwa ilibidi wahanga waliokuwa wanapata mateso chini ya utawala wa Nazi ulioongozwa na mbabe aliyefahamika kama Adolf Hitler nchini Ujerumani kuwa inabidi ifanywe mipango na warudi nyumbani, hakuwa na uhakika ni idadi gani ya watu itawasili katika viunga vya miji yao ila cha msingi ilikuwa ni kuwarudisha watu kwenye nchi yako ili kufanya kile walichokiita ?€˜?€™kupigania uhuru wao?€™?€™.

Katika kipindi hiki Hanagah ilikuwa ni moja ya shirika la kijasusi makini sana katika ardhi hiyo takatifu ulimwengun katika nchi zote za mashariki ya kati. Na katika mwaka 1945 Hanagah chini kitengo chake kinachohusika na upatikanaji wa silaha, kilifanikiwa kupata silaha nyingi Kaskazini mwa Afrika katika vita kuu iliyokuwa inaendeshwa na Italia na Ujerumani, siliha hizo kwa umakini chini ya wanajeshi wa kiyahudi zilipelekwa na kufichwa katika mapango Israeli katika eneo linalodaiwa kuwa shetani alimjaribu Yesu mara tatu lakini akashidwa.

Baada ya kupigwa kwa Japan mwaka 1945 makomandoo wa Israel waliokuwa vitani kipindi hicho walirudi nchini kwao kuongeza nguvu na ujuzi wao kwa Hanagah. Mwaka 1946 chini ya Ben-Gurion ilitoka amri kuwa sasa ni wakati kuwa na utawala kamili wa aridhi yao kwa kupigana na yeyote atayegusa maslahi yao na hapo walidhamiria kupigana na waarabu na waingereza wote kwa pamoja. Japo waisraeli walijua kuwa ni karata ya hatari kuicheza ila waliona hakuna budi kufanya hivyo kwa ajili ya uhai wa taifa lao. Katika vita hiyo wanajeshi wengi wa Uingereza waliuwa na vijiji vingi vya wapalestina vilipigwa kiberiti na wakabaki wanashangaa wingi huu na nguvu ya wa Israeli imetokea wapi?

Waingereza na waarabu katika eneo hili walikunatana na nguvu wa wayahudi ambayo hawakuitarajia na wasingezewa kuhimili hali ile zaidi na mnamo mwaka 1949 waingereza waliamua kuondoka eneo hilo la mashariki ya kati na kurudi kwao na masuala yote ya usimamizi wa nchi hizo yakaachwa chini ya usimamizi wa umoja wa mataifa (UN).

Kutokana na maadui sasa kuwa mbali kidogo ndipo Ben-Gurion alipoamua kutengeneza shirika la kijasusi imara litakalo kuwa na watu makini na wenye akili katika kulinda na kutetea maslahi ya Israel. Kutokana na kwamba Hanagah ilikuwa kama imegawanyika kutika harakati zake nje ya mipaka ya Israel, ambapo mawaziri na mabalozi wake walipendekeza vitu walivyopenda wao ndio vifanywe na shirika hilo. Hali hiyo ilionesha kuwa ya hatari kwa uhai na maslahi ya Israel ndipo mnamo March 2, 1951 kiongozi wao huyo alisikliza mapendekezo yote na akaamua kuwa nchini Israel kutakuwepo na shirika moja imara, litakalo fanya kazi kwa umakini na ustadi wa hali ya juu kuiweza nchi kuishi milele katikati ya msitu wa maadui ambao umewazunguka na shirika hilo la kijajusi litailinda Israel kwa njia yeyote ile na shirika hilo litaitwa Ha Mossad le Teum, ?€œthe Institute for Coordination.?€? Maarufu kama Mossad.

Tutajuzana mengine zaidi kuhusu kazi za Mossad.
 
shukrani mkuu!wengine hatujafatilia kitabu hvo tuko pa 1!endelea kutiririka
 
MOSSAD is Terrorist Killing Machine

Mkuu labda ungetoa definition ya terrorism then tukaangalia matendo yao compared na wengine coz mi huwa naona kama Intelligence zote ulimwenguni zinafanya vitu vinavyofanana ili kulinda nchi zao
 
Mpaka unefikia imri huu bado tu unatafuta tafsiri ya Terrorist hii ni ajabu sana
 
Mpaka unefikia imri huu bado tu unatafuta tafsiri ya Terrorist hii ni ajabu sana

Sidhani kama unakumbuka juz juz neno hili lilivyoleta tafran bungeni. Sikatai wala kukubali concern yako mkuu, ila ukiuchukulia ugaidi km unavyouona utaingiza waliopo na wasio Kuwepo
 
Wewe unavyojua UGAIDI NI NINI???
Sidhani kama unakumbuka juz juz neno hili lilivyoleta tafran bungeni. Sikatai wala kukubali concern yako mkuu, ila ukiuchukulia ugaidi km unavyouona utaingiza waliopo na wasio Kuwepo
 
Wewe unavyojua UGAIDI NI NINI???

Hakuna haja tubishane tuelimishane tu, na wala sina jibu kamili wala moja kwa moja ila nitafanya ninavyojua nitapata jibu bt uki condem hivyo ni sawa na wengine kuhusisha dini wa uislam na ugaidi kitu ambacho hakiwi sawa sana
 
Tukio la Morogoro kukamatwa watu wakiwa na mabomu ndani ya msikiti na Polisi walitaka kuwakamata polisi mmoja alijeruhiwa na Jambia sasa hao watu waliokamatwa ndani ya huo msikiti watashitakiwa kwa kosa gani??Kosa la kukutwa na silaha kinyume na sheria au kumzuia Polisi kufanya kazi yake au kujeruhi Polisi??au UGAIDI?? ila kwa maoni yangu kuna dini moja inajiita ya AMANI dini hiyo hukumbatia UGAIDI yaani kwao UGAIDI ni SAMAKI na MAJI.
Hakuna haja tubishane tuelimishane tu, na wala sina jibu kamili wala moja kwa moja ila nitafanya ninavyojua nitapata jibu bt uki condem hivyo ni sawa na wengine kuhusisha dini wa uislam na ugaidi kitu ambacho hakiwi sawa sana
 
GORDON THOMAS ndiye mwandishi wa kitabu cha GIDEON SPY. NI MWANDISHI MZURI WA HABARI ZA KIJASUSI.
Katika Kitabu hiki kuna Mambo 2 nimependa na sie kama nchi hasa wadau wa usalama wanapaswa kuzingatia:-
1. Daima dayama ujasusi uliobora hutegemea vyanzo vyake vikuu ni watu wala si technolojia( HUMINT - Human Intelligence(
2. Kama kawaida Siasa mbovu Ndiyo chanzo cha Kudolola kwa usalama wa nchi, hasa mtawala anapoingia madarakani na U Director of Intelligence. ambaye hana uzoefu wa kutosha kwenye combat operation.

MAMBO MEGINE YA KUSISIMUA AMBAYO YAMEJITOKEZA NI:-
- Kumbe magonjwa mengine sio majanga ya asili au ya Mola ni maradhi yanatengenezwa na watu kama siraha dhidi ya maadui zao, vimelea vya TB, EBOLA NA KIMETA(Anthrax).
-PP kitu muhimu sana kwenye ujasusi,( Psychological Profile) hizi ni taarifa za siri za viongozi wakuu wote nchi mbalimbali,wanapenda nini, chuki zao juu ya mambo fulani, strength zao na weakness zao katika maamuzi, mambo yao ya faragha, wanapenda kufanya nini faraghani,wanaudhaifu upi kimaumbile na kimaadili.. Taarifa hizi hukusanywa kwa siri kubwa na MOSSAD na kutunzwa kama future weapon dhidi ya mtu fulani ambaye anaweza kuhatarisha maslahi ya israel abroad. cf. Kilichomtokea Father Makarios wa CYPRUS... nikipata muda nitaelezea jinsi PP ilivyotumika kuharibu msimamo wa Askofu huyu mhafidhina. Thanks.

-
 
Back
Top Bottom