Hiyo inawezekana Mkuu,ila kwa sheria za utumishi cheo chako kinaanza upya. Kwa maana umeingia kazini na cheo cha HR Officer II, na elimu ya Degree, na umekitumiaka kwa miaka ile minne then umepanda na kuwa HR Officer I.
Sasa kama umeenda kusoma fani nyingine, then unataka kubadilisha ile kazi yako kutoka HR kwenda ICT labda, kama umesoma tena Degree, basi cheo chako kitashuka kutoka Officer I na kuanza upya cheo cha muundo cha Degree ambacho ni ICT Officer II.
Na kama umeenda kusoma Diploma, basi cheo chako kitashuka kutoka Officer I, kwenda ICT Technician II.
Ushauri, kuama taalumu inaleta maana kama mwanzo labda umeingia na Diploma then umeenda kusoma Degree, hapo moja kwa moja cheo chako kitapanda.
Inaleta maana tena kama umeingia kazini , na ndani ya mwaka mmoja tu ukiama taalumu, basi hapo hakuna issue, cheo hata kikianza upya hakuna noma kwasabubu umekitumikia ndani ya muda mfupi.
Ila kama cheo umekitumia kwa muda mrefu, na tena umeenda kusoma level ya elimu ya chini/level ile ile kwa kweli hiyo ni hasara kubwa, otherwise kipendacho roho na una uhakika unapoenda utatoboa.
Cha mwisho kabisa, kama unaweza kuama kitengo, na cheo chako kitaendelea kuwa hiko hiko basi hakuna tatizo, manake cheo kitaendelea kama kawaida. Hii inaFavor watu ambao taasisi zao ni kubwa kidogo na zina vitengo vingi. Kwa mfano wewe ni ICT OFFICER wa IDARA ya ICT, ila kuna idara nyingine inaitwa FINANCE Department, ila wanakitengo cha IT System Audit, unaweza kuamia kitengo cha Finance then unaenda kufanya hiki kitengo cha ICT, maana yake utaendelea kuitwa ICT Officer, kwahyo utaama na cheo chao.