Kubadili jina kwa mtumishi wa Serikali

Kubadili jina kwa mtumishi wa Serikali

Jendahyeka

Member
Joined
May 17, 2021
Posts
46
Reaction score
122
Habari za majukumu wana JF bila kuzunguka zunguka naomba kufahamishwa endapo kuna uwezekano wa mtumishi wa serikali kubadili jina moja katika majina yake matatu na yakaweza kubadilika hadi katika salary slip zake

Mfano:
mtumishi anaitwa Chipindi Justine Makoloka

Anataka kubadili na aitwe Frank Justine Makoloka

Kwenye cheti chake cha kuzaliwa aliandikishwa majina mawili
Frank, Chipindi (Name of any)

Sababu kuu ya kubadili hili jina ni kutokana hitilafu za kifamilia hasa kwenye swala la kiimani yeye hayupo tayari kuabudu mizimu na wenyewe wanasema yeye Ndio Chipindi kwa kuwa hata riziki yake anaipata kwa kutumia hilo jina la Chipindi.

Naomba mnisaidie kujua huyu mtu kama anaweza kubadili hili jina na ukizingatia kwenye cheti chake cha kuzaliwa yapo majina yake yote mawili. Frank na Chipindi.
 
Huwezi kukimbia majukumu yako kwa kujibatiza jina jipya.

Safisha mapito yako ili uvalishwe ngozi na roho mpya.

Sent from my SM-J320H using JamiiForums mobile app
 
Another brainwashed creature anakimbia asili yake..soon wazungu watakuomba ndogo..kwakua una mahaba nao huwezi wanyima.

Heshimu na linda majina ya ukoo mana bila hao usingekuwepo.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona mambo ya kawaida kurithishwa imani ya mababu zetu, au mkuu unafikiria utakua mganga au utaanza kupaa na ungo hapana si kweli.

Ata ukibadiri jina haita saidia kitu, jamii yako itaendelea kukutambua chipindi tuu.

Atakama unaamini kazi hujapata kupitia ilo jina, ila amini zengwe zipo unapigwa na ukoo hutoboi tena kudadeki. Ulozi wa ndugu wa damu ni hatari kuliko wa mbali.
 
Mkuu kubadili jina la mwanzo inakuaga ngumu kidogo, itakuja kukusumbua tu, labda majina ya wazazi hapo sawa.
Mfano mzuri ni mie hapa, baba yangu ni mkristo na mama yangu ni muislamu, na mie ni muislamu, nimesoma primary mpaka chuo nimehitimu kwenye vyeti nilikua natumia Ubin wa baba yangu (mkristo), but mwaka juzi nikaamua kubadili Ubin wa baba nikaanza kutumia Ubin wa mama yangu (muislamu) ili mradi tu majina yangu yasiwe na mkanganyiko wa uislamu na Ukristo.

1.Nilitafuta mwanasheria akanitengenezea hati ya kubadili majina (Deed Poll)
2. Nilipeleka hiyo deed poll wizara ya Ardhi kule posta then nikalipia 32k ili jina langu jipya lisajiliwe rasmi, then after two weeks nikaenda kuchukua deed poll yangu ikiwa tayari imeshagongwa Muhuri wa wizara ya ardhi.
3. Kilichofuata nikaenda pia na kwenye ofisi za NIDA kupeleka taarifa zangu japo kule NIDA kunakuaga na complications nyingi sana especially kwa mtu ambaye tayari anakitambulisho cha NIDA kinachosomeka kwa lile jina la awali tofauti na mtu anayeenda kujiandikisha.

Inshort ni hayo tu kwa experience yangu mie Boss
 
Hilo linawezekana. Onana na wakili au fika Mahakamani uandikiwe hati ya deed poll, vigezo na taratibu utaambiwa hukohuko.
 
fika ofisi ya mwanasheria aliye karibu nawe... pia kama una marafiki walio soma taalma hii ya sheria wana weza kukupa msaada wa awali
 
Mkuu kubadili jina la mwanzo inakuaga ngumu kidogo, itakuja kukusumbua tu, labda majina ya wazazi hapo sawa.
Mfano mzuri ni mie hapa, baba yangu ni mkristo na mama yangu ni muislamu, na mie ni muislamu, nimesoma primary mpaka chuo nimehitimu kwenye vyeti nilikua natumia Ubin wa baba yangu (mkristo), but mwaka juzi nikaamua kubadili Ubin wa baba nikaanza kutumia Ubin wa mama yangu (muislamu) ili mradi tu majina yangu yasiwe na mkanganyiko wa uislamu na Ukristo.

1.Nilitafuta mwanasheria akanitengenezea hati ya kubadili majina (Deed Poll)
2. Nilipeleka hiyo deed poll wizara ya Ardhi kule posta then nikalipia 32k ili jina langu jipya lisajiliwe rasmi, then after two weeks nikaenda kuchukua deed poll yangu ikiwa tayari imeshagongwa Muhuri wa wizara ya ardhi.
3. Kilichofuata nikaenda pia na kwenye ofisi za NIDA kupeleka taarifa zangu japo kule NIDA kunakuaga na complications nyingi sana especially kwa mtu ambaye tayari anakitambulisho cha NIDA kinachosomeka kwa lile jina la awali tofauti na mtu anayeenda kujiandikisha.

Inshort ni hayo tu kwa experience yangu mie Boss
Nashukuru mkuu kwa ushauri mzuri
 
Back
Top Bottom