Kubadili Timing belt + Gear box oil etc

Kubadili Timing belt + Gear box oil etc

muzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2016
Posts
1,041
Reaction score
1,457
Habari za muda wapendwa,
Karibuni katika uzi huu, kwa wale wazoefu wa vyombo vya moto, hebu tupeane uzoefu kuhusu kubadili yafuatayo kwenye gari zetu. Ni wakati gani au km ngapi unatakiwa kubadili vitu hivi. Pia si mbaya ukiongezea na others ambayo inakwenda sambamba ya hizo liquid
  1. Timing belt
  2. Gear box oil
  3. Difu oil
  4. Coolant
  5. Others
 
1;Timing belt inatakiwa ubadilishe kila baada ya km 100,000.
2;Gear box oil inategemea ni gear box ya automatic au Manual,kama ni automatic badilisha kila unapobadilisha Engine oil 3000km to 5000km na kama ni manual utakuwa unaongezea tu kama imepungua hata mwaka poa tu na Difu vile vile
 
No 2. Gear box oil ya Automatic yaani AUTOMATIC TRANSMISSION FLUID ( ATF ) haibadilishwi kwa hizo kms ulizotaja mkuu, inabadilishwa kati ya kms 50,000 na Kms 100,000 kutegemeana na hali ya ubora wake unavyoonekana kwa macho, yaani mpaka iwe nyeusi ndio unabadilisha. Rangi yake ya asili ni nyekundu.

No. 3. Diff oil pia vilevile ni kuongeza tu. Coolant pia haibadilishwi labda kwenye Kms 100,000+

cc muzi
 
Hapo kwenye gear box oil kizungu zungu nishaamua after 10, 000 km nitakuwa nabadilisha naona kila mtu anaongea lake na manual ilikuja ya kichina.
 
Hivi majuzi nilikuwa kwenye mkutano wa SAE nikapiga kelele sana kuwekwa kwa standard kuwa magari yote yawe yanatumia timing chain badala ya timing belt. Hata hivyo utashangaa sana kusikia jinsi mainjinia wengine wanavyotetea timing belts hizo; walikuwa na sababu ambazo ni sahihi kiufundi ingawa zinaleta contradiction kwa vile kuna magari mazuri mengu tu yanayotumia timing chain. Nyumbani kwangu magari mawili ni ya timing belt, na nimekuwa nayahesabia muda wa servise kwa karibu sana, wakati magari mengine mawili yanatumia timing chain ambayo hayako katika mahesabu yangu ya service. Ingekuwaje iwapo tusingekuwa na wasiwasi wa timing belts katika magari yetu. Miaka kumi na nne iliyopita nilimshuhuduia dada mmoja akipata ajali mbaya sana kwa sababu timing belt yake ya Honda Accord ilikatika akiwa katikati ya safari!
 
Kuna rafiki yangu alidanganywa na fundi wake kuwa hiyo gear box oil haitakiwai kubadilishwa,alikaa nayo mpaka ilipokaribia kufikisha km 10,000 gari ikawa na shida ya kubadilisha gear,tatizo hili lilimsumbua sana mpaka akaamua kuuza gari yake.Na ni kweli kila fundi ana maelekezo yake kuhusiana na hii oil,tunahitaji mtaalamu/fundi aliye bobea atufafanulie hil kitaalamu zaidii wadau.
 
Kuna magari hayana cock ya kumwaga hiyo transmission fluid (mfano- toyota mark x) mafundi wanadai utumie tu maana transmission iliyowekwa japan ni orijino, inakuwaje hapa? Oil hii inamwagwa vipi kwenye magari ya namna hiyo? Hata stick ya kupima huwa haipo kabisa
 
Kosa kubwa ni uelewa mdogo. Kila gari ina specification zake za gear box oil, ukikosea kuweka oil unaua gear box, kwa mfano automatic (atf) ziko nyingi cha msingi usome stic ya gear box imeandikwa no gani. Pili huwa haibadilishwi hovyo huyo anayekuambia kubadilisha kila baada ya service hayuko sahihi kabisa. Soma driver manual ya gari itakupa maelezo sahihi, pili unaweza ku google kwa kutumia model no ya gari itakupa majibu
 
Ni sawa kabisa unapoweka oil ambayo sio iliondikwa kwenye stick performance yake inakuwa sio nzuri.
 
Back
Top Bottom