Kubadilibadili wateule kama kubadili suti hakuna tija

Kubadilibadili wateule kama kubadili suti hakuna tija

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Tangu serikali ya awamu ya sita iingie madarakani inaelekea kazi ya kuteua na kutengua imegeuka kama sehemu mojawapo ya majukumu muhimu sana ya serikali hiyo.

Mpaka imefikia hatua wananchi wanashindwa kuelewa haswa viongozi wao wa wizara, na taasisi mbalimbali ni akina nani. Maana imegeuka kama fasheni vile, kutwa kuteua kuchwa kutengua. Mpaka wananchi wanajiuliza mteuaji anataka kitu gani haswa?

Kinachoshangaza, wanaoteliuwa katika wizara fulani unakuta wamewahi kutumbuliwa katika wizara hiyo kisha baada ya miaka michache wanateuliwa tena katika wizara hizohizo.

Sasa unajiluza hivi tatizo lilikuwa ni la waliotumbuliwa hapo awali au tatizo ni la mteuaji?, maana haiwezekani ukaona mtu hafai kuhudumu katika nafasi fulani halafu baada ya muda ukaona anafaa zaidi kuhudumu ktk nafasi hiyohiyo. Hii maana yake huenda wewe mteuaji ndiye mwenye tatizo!

Kibaya zaidi ni kwamba inaonekana hizi teuzi zina mrengo wa kisiasa kuliko tija ya kazi, maana mara kadhaa hutokea kipindi kuna joto la kisiasa sasa ili kubadili upepo wa kisiasa hizi teua tengua hutokea.

Tangu tupate uhuru, Samia amevunja rekodi ya teua tengua mpaka mtu unajiuliza anataka nini haswa?. Pengine kitengo chake cha vetting kina matatizo, kama siyo tatizo la kitengo cha vetting basi yeye mwenyewe ndiye mwenye matatizo, na si matatizo kidogo! maana haiwezekani kila siku ni kuteua tu, sasa sijui anatengua ili iweje kama anaowatengua kesho anawaona wanafaa!. Absurd!

Na hii itoshe kutuonyesha kuwa tatizo kuu ni mifumo kuliko watu, maana laiti ingalikuwa tatizo ni watu basi Samia asingekuwa anateua walewale aliowatumbua juzi.

Laiti tungeona Samia anafanya reforms kwenye mifumo ya nchi kwa kasi kama hii ya teua tengua tungeona kuwa anafanya la maana. Lakini haya ya kurecycle makada walewale ili kununua loyalty ndani ya chama, au kubadili gumzo la kisiasa nchini, kunamfanya Samia mwenyewe aonekane ni rais anayeyumbayumba, ambaye hata kupanga timu yake mwenyewe kunamsumbua.

Ushauri kwa Samia. Ni heri uwe unavunja baraza la mawaziri kisha ulisuke upya kuliko hii ya kila siku ya kubadilibadili watu kama unabadili suti vile. Haina tija na inakufanya kuonekana dhaifu na wananchi wanapuuza hizi teua tengua maana zimekuwa too much bila kuona mabadiliko yoyote ya maana ktk maisha yao!
 
Ni dalili hajui anataka nini, anaenda wapi, anatafika vipi, malengo yake ni wapi? Urais anauchukulia kama mchezo fulani hivi wa rede. Hayuko serious kwa maslahi ya Taifa, yupo serious kwa maslahi yake binafsi na kuendelea kuwa Rais.
 
Tabu sana
 
Nadhani kuna tatizo katika mchakato mzima wa teuzi au wakisha teuliwa haweelewi majukumu yao ni nini. Au chugio la Mama ni kali mno.
Au hupo ubadilifu ambao huwa hauna msamaha kisiasa.
Lakini kama hawafai kwanini anawateua tena au anawabadirishia majukumu?

Tukiacha uzembe wa mtu mmoja mmoja, kwanini kiongozi mkuu anasafiri na lundo la mawaziri,makatibu wakuu na wasaidizi wao mikoani kwa kazi tu ya kutia jiwe la msingi au kufungua taasisi husika.
Hiyo ni misappropriation ya nguvu kazi ya wasaidizi wa Raisi.
Mikutano ya hadhara isiokatika nayo ni matumizi mabaya ya muda wa kujenga taifa.Tujisahihishe.
 
Wanaugeza uongozi kama ucelebrity badala ya kushughulika na umasikini wa wananchi
 
Back
Top Bottom