Kubadilika kwa magnetic poles za dunia, North kuwa South na South kuwa North

Kubadilika kwa magnetic poles za dunia, North kuwa South na South kuwa North

dosho12

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
596
Reaction score
1,475
Hivi unajua kuwa dunia ina North pole mbili na South pole mbili, ambazo moja ni za magnetic na zengine na za geograpic.
images.jpeg


Magnetic North poles na South pole ndizo zinazosaidia kwenye kuzuia mionzi hatari iliyopo kwenye space na solar flares zilizo kwenye jua.
How-Earth’s-magnetic-field-protects-us-from-solar-radiation.jpg


Sayari kama Venus na Mars zenyewe hazina magnetic poles ila dunia inayo haija julikana ni kwanini sayari nyingine hazina magnetic pole ila kunauwezakano sababu ikawa kwenye Core ya dunia ambayo inafanya kazi kama dynamo kwa kuwa kwenye outer core kuna chuma iliyo kwenye mfumo wa liquid ukumjuisha na madini ya nikel na pia kwa kuwa inner core kuwa katikati ndani ya dunia kuna pressure kubwa na kusababisha.
images (1).jpeg


Kuwepo na electrical charges zinazoflow kwenye core na kisha kutengeneza magnetic field na kwa kuwa earth core inazunguka inasababisha magnetic field zisi sambae na kuflow pande mbili tu ambazo ni north na south.

Hizi magnetic poles kwa kawaida huwa zinabadilika ambapo north inakuwa south na south inakuwa north na inasemekana ilishatokea hivyo kipindi cha miaka 780,000 iliyopita. Na inasemekana earth core imeshaanza kupunguza spidi yake

Kuna uwezekano kwa mara ya kwanza kwenye historia ya uwepo wa binadamu wakashuhudia kubadilika huko ndani ya miaka kama elfu ijayo, kinachotisha sio kubadilika kwake ila ni mchakato wa kubadilika huko sababu zikiwa zinabadilika magnetic fields inayotulinda na mionzi inapungua nguvu kwa takribani asilimia 90% na kusababisha madhara makubwa kwenye dunia.

Kama vile magonjwa ya kansa tokana na mionzi pia wanyama kama ndege na nyangumi wanaotumia muelekeo wa magnetic watahangaika, kufeli kwa power grid za kuzalisha nishati kama umeme sababu power plant hutumia sumaku kubwa kutengeneza umeme satelite zitashindwa kufanya kazi na kuharibika.

Cha kushukuru madhara hayata kuwa makubwa sana kwenye mionzi kwa kuwa bado dunia ina ozone layer itayotukinga na mionzi kwa muda kwa kuwa mchakato wa kubadilika kabisa huchukua mpaka miaka elfu saba

Cha kuongezea hivi unajua kuwa sayari ya venus inazunguka juu chini tofauti na sayari nyingine hivyo hii hufanya ionekane kama inazunguka clockwise kwenye muhimili wake
images (2).jpeg


wakati sayari nyingine huzunguka counter clockwise inasemekana haya ni madhara ya kugongana na vimondo vikubwa hivyo hufanya venus kuzunguka juu chini na clockwise kwenye muhimili wake na pia kufanya jua kwenye sayari hiyo kuchomoza upande wa magharibi.

Wanasayansi wanahisi huenda siku za mbele dunia ikagongana na vimondo vikubwa kama vilivyo tokea zamani na kuna theory huenda dunia ikaja kuwa kama venus ikageuka juu chini, na hii ni theory tu kwenye imani ya dini ya kiislamu na baadhi ya wakristo wachache wana amini siku za mwisho jua litachomoza magharibi huenda kukawa na muunganiko wa haya matukio, hayo ni kwa maoni yangu.
 
Hmna hayo mambo ya kwenda mwezini wala solar system. Wajuzi wa mambo wanasema dunia imefunikwa na firmament mtu hawezi kutoka wala kuingia. Kafatilie mselezo

View: https://vm.tiktok.com/ZMhqG1DUS/

View: https://vm.tiktok.com/ZMhqG6QcE/

View: https://vm.tiktok.com/ZMhqGSBKb/

Inaweza kuwa kweli ila inakosa uhalali kwa sababu ushahidi wa kutoka nje ya dunia upo mwingi.
Hivi unakumbuka kile chombo Apollo ambocho mpaka leo tokea miaka ile ya 70 kinandeleea na safari, kipo nje ya dunia kwa umbali mrefu mno.
 
Shida inaanzia pia tutataka kujua behind hiyo intelligence kuna nini?
Yes, na tukiigundua tutataka kujua behind hiyo int kuna nini tena so it will never end.

Lakini hii haifuti nadharia kuwa ipo too perfect, yaani ni kama kuna ulinzi kabisa upo kuilinda dunia. Mfano uwepo wa Jupiter, mawe makubwa na majabali yote yanayokuja ukanda huu yanavutiwa Jupiter na nguvu yake ya mvutano, isingekuwepo dunia kila wakati ingevamiwa na majabali na pengine maisha yasingekuwepo.
 
Vipi kuhusu vimondo vinavyoanguka duniani mfano kile Cha mbozi na maneno mengine duniani. Vimetoka wapi???
Kuna video hapo juu. Inasema wamefanikiwa kupasua Hio firmament matundu. Wanachokifanya ni kutuma rocket na nuclear kupasua huo uzio. Madhara yake ndo hayo
 
Yes, na tukiigundua tutataka kujua behind hiyo int kuna nini tena so it will never end.

Lakini hii haifuti nadharia kuwa ipo too perfect, yaani ni kama kuna ulinzi kabisa upo kuilinda dunia. Mfano uwepo wa Jupiter, mawe makubwa na majabali yote yanayokuja ukanda huu yanavutiwa Jupiter na nguvu yake ya mvutano, isingekuwepo dunia kila wakati ingevamiwa na majabali na pengine maisha yasingekuwepo.
Hapa ni kukataa concept kwa kutumia concept unayoikataa🤔
 
Mpaka leo swala la main source of Earth magnetic bado halijatambulika though baadhi wanausisha na movement ya mantle.
 
Back
Top Bottom