Kubadilisha ATF

Makobus

Senior Member
Joined
Jul 30, 2012
Posts
169
Reaction score
110
Habari wataalamu. Ukiangalia maelekezo ya utunzaji wa gearbox ya hizi gari za kisasa yaliyopo kwenye dipstick (automatic) yanasema kuwa kwa hali ya uendeshaji wa kawaida wa gari, hakuna haja ya kubadilisha ATF. Kutokana na hilo:-

1. Uendeshaji wa kawaida ni upi?
2. Kuna madhara yoyote nikiamua kubadili baada ya kwenda km kadhaa hivi.
 
Normal driving condition, ni ule uendeshaji wa kawaida kabisa wa mtu wa kawaida, gari ikiwa inabeba mzigo na abiria kwa idadi na uzito uliokadiriwa kutoka kwa mtengenezaji.

Ukifanya racing, ambulance, towing, safari ndefu sana, n.k unakuwa unafanya kitu ambacho kinavuka matumizi ya kawaida, na pengine mtengenezaji hajakadiria impact yake.

Kama gari yako imeandikwa hivyo kwenye dipstick na matumizi yako ni ya kawaida sishauri kubafilisha hiyo ATF.
 
Endapo imekua ni nyeusi sana mithiri ya engine oil jee?
 
Endapo imekua ni nyeusi sana mithiri ya engine oil jee?
Hapo huna namna ni kubadili tu, kuna uwezekano hilo gari huko lilikotoka halikutumika kwa namna ya kawaida
 
hili swala lilishajadiliwa sana humu ila ni ngumu kupata jibu mahusihusi kama una hela na unaona umetembea KM zakutosha eg. 50,000+ na unaona kabisa gear box haibadilishi gear kama ilivyokua zamani we imwage weka mpya ya aina hiyo uliyotoa (Genuine na right type). Hawa wenzetu hesabu zao nyingi wanapigiaga mpaka mwisho wa Manufacture Warranty na baada ya hapo Gari inakua assumed ni yakubadilisha...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…