Salute kwa wanajamvi wote! Ktk dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia kuna mambo mengi yanafanyika, mengine ya kushangaza. Kuna hili la kubadili jinsia, naomba tuwekeane sawa hasa kwa wenye kufahamu vizuri kwa faida ya wengi. Inakuwaje mwanaume kubadilishwa jinsia? Je, ataweza kubeba mimba? Vp kuhusu mabadiliko mengine ktk mwili kama ndevu, sauti, hormones n.k? Maana nimeshutushwa na tetesi za Mike Tyson kuwa kajibadilisha jinsia na kuwa mwanamke. Na pia mwanamke anaweza kubadishwa kuwa mwanaume?; vp kuhusu mabadiliko kama hormones n.k? Samahani kama hii mada ilishawahi kujadiliwa humu. Nawasilisha. Asanteni.