Kubadilishwa kwa kikosi cha Yanga jana

changaule

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2020
Posts
6,039
Reaction score
10,151
Jana mashabiki wa Yanga wameumia sana kwa kitendo cha kocha wa Yanga kupanga kikosi B dhidi ya Gwambina na lawama zote zimeelekezwa kwa kocha. Kwa kuangalia kwa jicho la tatu, unaona kabisa ya kwamba huu mpango huenda ikawa viongozi wa yanga wamehusika katika kumshauri kupangwa kwa hiko kikosi.

Tensheni ya mechi ya Simba na Yanga, huyu kocha hajui lolote. Lakini kiutamaduni wa hizi mechi za watani wa jadi wanaujua zaidi waliokuwepo kabla ya yeye kocha kuwepo (kocha msaidizi + viongozi). Ni vigumu sana kwa kocha yeyote mgeni asiyepata kupewa historia ya usimba na uyanga akafanya vile.

Na ndivyo ilivyozoeleka miaka yote kuwa, mechi ya Simba na Yanga viongozi na washabiki wanakuwa na tensheni kubwa utafikili ukiweza kumfunga mwenzio utapata alama sita ama ndio kombe unachukua hapo hapo. Tabia ya viongozi kuingilia majukumu ya kocha katika mpira wetu wa kibongo hili lipo sana. Makocha wanakuja kufundisha Yanga ama Simba lakini maamuzi mengi ya upangaji wa kikosi yanafanyika kwa mashinikizo. Jana kocha mpaka kuamua kuchezesha kikosi kile, kuna vitu kaambiwa, ama kushauriwa na viongozi.

Kwa namna Yanga inavyoendeshwa kiswahili hivi sitoshangaa kubadilisha makocha kila mara, kwasababu madhaifu ya kiuongozi yanafichwa katika kivuli cha makocha.

Msimu ulioisha mechi ya Simba na Yanga katika kombe la Azam, hii mechi waliosababisha Yanga kupata kipigo cha goli nne ni hawa hawa viongozi ukijumlisha na washabiki. Kabla ya mechi mashabiki wanauliza Morrison vipi, Tshishimbi nae vipi, Niyonzima nae vipi tunataka kujua hali zao watakuwepo kwenye dabi? Hili limewapa presha viongozi na mwisho wa siku kushinikiza kwa kocha kufanya kila namna hili hao wachezaji wasikosekane kwenye dabi.

Pengine kocha angeachwa afanye kazi yake kwa kuzingatia kiwango cha utimamu (fitness) wa mechi husika, Yanga wasingepoteza ama wasingefungwa magoli yote yale.

Viongozi pamoja na washabiki, tuache kuingilia majukumu ya kocha. Tunajua kuwa mwenyekiti anataaluma ya ukocha lakini embu tujenge mazingira ya kumpa uhuru makocha.

Tukija kwenye mchezo wenyewe wa jana ni kwamba tatizo la Yanga bado ni lile lile tu, hata wangeingia kikosi cha siku zote bado lisingeondoa tatizo lililopo katika kikosi cha Yanga. Yanga ya kikosi kilizoeleka kilikuwa kinaahindwa kutumia nafasi zinazopatikana na kupelekea kupata ushindi mwembamba kwa kila mchezo wanaocheza.

Kikosi kamili cha Yanga kisingefanya kitu tofauti na kikosi B kwasababu mastraika wa Yanga ndio walewale wa siku zote. Nafasi jana zimetengenezwa nyingi tu lakini wachezaji wamekosa umakini kwa kushindwa kuzitumia.

Kikosi kamili cha Yanga kilikuwa kinashinda kwa mbinde mno sasa unakuja kupambana na Gwambina ambao ni wazuri wa kukaba ambapo tumeona hata Simba pamoja na kuwa na mastraika wazuri lakini alipata tabu kufungua ukarasa wa magoli mpaka wakapata magoli kwa njia ya faulo na kona ni vipi hii yanga uliyokuwa na ubutu wa mafowadi waje waifunge Gwambina?
 
Unapumzisha wachezaji muhimu afu mnakuja kupigwa kipigo kizito
 
Acheni visingizio,huo ndio uwezo wenu ulikokomea.Utopolo hakuna mchezaji wa maajabu.Hao akina Sarpong mmeshaanza kusema hawana viwango vikubwa.
 
Acheni kuwashinikiza. makocha alafu mwisho wa siku mnakuja kuwalaumu...



Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…