Kuna tetesi kuwa Saed Kubenea, mhariri mkuu na mmiliki wa gazeti pendwa la MwanaHALISI naye ni miongoni mwa waandishi wa habari walionunuliwa na Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge kwenye mkakati wa kuzuia mafisadi hawa wasifutwe uanachama wa CCM.
Tetesi ziliopo ni kuwa Kubenea kapewa pesa na mali kadhaa zenye thamani kubwa ili gazeti lake la MwanaHALISI liache kabisa kuwaandika habari yoyote mbaya (negative) kuhusu kina Rostam, Lowassa na Chenge tangu CCM ilipowataka wajitoe wenyewe kwenye uongozi.
Pamoja na kupigwa marufuku kuandika habari zozote mbaya kuhusu Rostam, Lowassa na Chenge, Kubenea pia amepewa kazi maalumu kuandika habari za kumchafua Rais Jakaya Kikwete, mtoto wake Ridhwani Kikwete, Samuel Sitta, Nape Nnauye, na viongozi wengine wa CCM.
Baada ya kuangalia mwenendo wa MwanaHALISI kwa wiki kadhaa na kuona ni kweli gazeti hili limekuwa na kigugumizi cha ghafla cha kuandika maovu ya Lowassa, Rostam na Chenge na badala yake linamshambulia Kikwete na Sitta kila kukicha, nimepata hofu kuwa huenda hizi tetesi si za kupuuza hata kidogo.
MUNGU IBARIKI TANZANIA!