Kubenea wa MWANAHALISI amenunuliwa na mafisadi?

Mimi kila wiki sikosi kusoma magazeti manne -- Mwanahalisi, Raia Mwema, Kulikoni na Dira. Haya ndiyo magazeti "huru" kwa maana halisi ya neno katika mazingira yetu ya Tanzania na yamekuwa yakijitahidi kueleza ubayana ufisadi unaoendelea nchini.

Ila kama wadau wengine walivyogundua, gazeti la Mwanahalisi limepoteza mwelekeo katika kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja sasa na sielewi haswa hii inatokana na nini. Tatizo la Watanzania ni wavivu kufikiri na kufanya uchambuzi. Pia ni wepesi wa kupuuza mawazo, fikra au hoja mbadala.

Hauhitaji kuwa rocket scientist wa NASA kubaini kuwa kuna mdudu ameingia Mwanahalisi katika kipindi hiki cha sasa. Ila sielewi kama mmiliki wa hili gazeti sasa ameanza kuwaogopa kina RACHEL au kanunuliwa.
 
sasa hapo tatizo ni nini? Ni kwamba ktk hizo habari zilizoandikwa JK kasingiziwa si za ukweli? Au hutaki jk aandikwe au tatizo lako ni nini hasa kwa hizo habari sijaona kununuliwa au kutumika kokote otherwise wewe una tatizo na watu fulani kuanikwa madudu yao na unataka watu fulani tu ndo waanikwe au?
 
Duuuh, hata sisi kwenye media tumekuwa tunajiuliza MWANAHALISI kulikoni? Mbona ghafla bin vuu imeanza kuwagwaya kina RACHEL na kumwandama Kikwete weeeee. Sisi tumezoea MWANAHALISI ambayo inatwanga kote kote without fear or favour. Kaka Kubenea tugawana basi hivyo vijisenti. Habari hizi zimetapakaa mitaani kuwa mambo yako freshi sana siku hizi za karibuni.
 
hatujali kuwa anatwang wapi, ila tunataka atwange kote, kama anavyoibua ufisadi wa kikwete ni sawa kabisa, ila asinyamazie ufisadi wa akina lowasa
 
Kwani hawa mapacha watatu wameibuka na jambo gani jipya?Au unataka waanze kuandika lolote tu hata kama halina maslahi kwa taifa?
Sitamani kuliona gazeti nilipendalo la mwanahalisi likiwa na vichwa kama;
1.Kumbe Regina ni MKE wa Lowassa!!
2.Rostam afumwa akila wali manzese.
3.Binti wa Chenge aolewa.
Mwanahalisi likifanya hayo hapo juu nitalidharau.
Tujitengenezee utamaduni wa kutumia UBONGO na sio TUMBO tunapofikiri.
 
hizo teesi za uongo.kuna matukio mengi yanatokea sasa ya nini habari iwe ileile?
watanzania sijui Mungu katulani!?..wewe ulishajua RACHEL ni mafisadi,kinachotakiwa ni sisi kushinikiza washitakiwe sio kuwa laumu mwanahalisi kana kwamba wana mamlaka ya kuwapeleka police.kama kuna jipya litatokea naamin wataandika.siyo waandike tu.kumbuka wanaandika habari zilizofanyiwa utafiti.kama mnataka udaku magazeti ya udaku yapo.kwani huyo kikwete anayeandikwa siyo fisadi?
 

Ukiangakia kweli unaona kuna trend/pattern hapa inajaribu kujengwa. Wakati habari kubwa tangu kikao cha NEC imekuwa ni Rostam Aziz na Chenge na Lowassa kutakiwa kufukuzwa CCM, MWANAHALISI kwa makusudi wameamua kupoteza mwelekeo na kula sahani moja na KIKWETE tu. Katika zaidi ya mwezi mmoja uliopita, Raia Mwema, KULIKONI na DIRA yamekuwa yakiwabamiza kina RACHEL kwani hiyo ndiyo habari kubwa ya sasa. Kumbe MWANAHALISI inaonekana wamepewa kazi maalumu na kina RACHEL.

Kwa mwenendo huu, nabashiri headlines za story za matoleo yajayo ya MWANAHALISI:

1. Kikwete sasa ajuta kumfukuza kazi Makamba

2. Kingunge amtaka Kikwete asifukuze kina RACHEL

3. Kikwete matatani tena

4. Lowassa tishio kwa Kikwete

BURIANI MWANAHALISI!
 
Lisemwalo lipo,kama halipo,lipo njiani linakuja...lkn pia tetesi za kumchafua kubenea zipo ili tu watu waache kuutafuta ukweli....ni uamuzi wake kuandika habari anayotaka iandikwe...hivi kila cku atawaongelea kina rostam tu?gazeti litachokwa na watu...mwacheni avumbue mengine....
 

Hapo kwenye red weka UHURU. Mwanahalisi halina siku nyingi kama unavyomaanisha.
 

Haaa inaelekea kuna ukweli hapa nini? ndo maana ninaiogopa sana siasa!!!
 
Guys,
MwanaHalisi liko juu pamoja na ukweli kwamba -ubenea hajaandika 'hot' news - hazipo.
INSTEAD OF READING KUBENEA'S ARTICLES kwa nini msimsome mzee Ndimara? Gazeti la wiki iliyopita alitoa kitu.
 
awachafue, awarembe haisaidii kwani mwisho wa yote umefika... Tanzania ijayo haijengwi ma magazeti bali wenye nia njema na nchi yao

afterall i dont see any impact ya kuremba wala kuchafua hayo makundi yote mawili. kama ningekua kubenea pesa zao ningekula na kazi ningefanya ninavyotaka

mnaandika hivyo ili ya nape kutukana wachagga yaonekane ni kampeni sio??

this time mmeula wa chuya
 

umeongea ukweli mkuu
 
Haaa inaelekea kuna ukweli hapa nini? ndo maana ninaiogopa sana siasa!!!
kamtandika lowassa for six years mmeona sawa, sasa leo kagusa presidaa mmeanza kelele sio?? kweli kuny@ anye kuku....
 
Kubenea yupo hapa jamvini naomba ajitokeze kujibu hizi tetesi, sio siri kati ya waandishi niwapendao Tz Kubenea ni mmjoa wapo kama nae kanunuliwa ni hatari kwa sekta ya habari Tz hasa habari za uchunguzi
 
Nafikiri Kubenea angejifunza kutoka gazeti la RAI,hapo mwanzoni lilipokuwa na akina Kubenea mwenyewe,na akina Ulimwengu lilikuwa ni gazeti ambalo kila mtu makini alikuwa na kiu ya kulisoma ,lakini baada ya kuanza kuandika habari za kuwatukza watu na kuandikwa kwa kufuatwa matakwa ya watu fulani na mmiliki wake tumeshuhudia RAI likiwa garasa na gazeti la kufungia vitumbua ,si muda mrefu MwanaHalisi nalo litakuwa gazeti la kufungia vitumbua
 

Yaani bongo inachekesha sana, enwayz nataka kulizungumzia hili kimantiki na si kishabiki. Sitetei wala sishabikii ununuzi wa mwandishi at least kama ni kweli. Mwanahalisi iliandika sana kuhusu habari za kina Lowassa to an extent kuna watu wakasema JK analitumia mwanahalisi, wakabezwa kuwa ni wazushi, wakatishwa na kupelekwa mahakamani. CCM ikawatetea, katibu mkuu "former" (Makamba) na JK wapo in records kuwatetea.

Leo CCM imekubali na imetangaza kuwachukulia hatua something Mwanahalisi has been advocating for the last four years. Mwanahalisi, wapinzani na wanaharakati wengine wanaweza kusema sasa wamewathibitishia wananchi kile walichokuwa wakikisema kuhusu hao akina RA, EL na AC.

Kinachofanywa na mwanahalisi sasa ni ku "move on" huku wakitizamia je kweli hatua hizo zitachukuliwa....... Wanakuwa more critical kwa JK kwa sasa kwa sababu habari kama RA au Lowassa kuwa mafisadi "is no longer news it is obvious", hata chama chao kimethibitisha. Magazeti kazi yake ni kuripoti news.

Hivyo basi kusema eti mwanahalisi wamenunuliwa wakati hao hao wanaosema hivyo wamekuwa wakikejeli gazeti hili kwamba ni kijarida cha mitaani, hakiaminiki na kinaokoteza habari inashangaza kidogo kama siyo sana. Na je tukifikiria objectively hayo yanayosemwa kuhusu JK hayana mantiki? Kwa mtizamo huo in maana mwanahalisi imenunuliwa pia na Mahalu, Mkapa, Zombe, Mkono, Idris Rashid, Jeetu Patel? What a craaaap!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…