Mkuu
GlorytoGod,
Pole, ..mara nyingi kutokwa damu nyeusi(huashiria kiwango kikubwa cha damu/damu iliyotoka kwa muda mrefu).
Matatizo hayo, yanaweza kutokea hasa wakati wa hedhi, ni vizuri kujua mzunguko wako ni siku ngapi, je unakuwa hedhi siku ngapi, kama kuna kuwa na damu inayotoka kati ya mzunguko na mzunguko? Je, kuna wakati damu hotoka kama "mabonge mabonge"?
Je, kizunguzungu, kukosa nguvu, wakati mwingine kupoteza fahamu(kuzimia) hutokea?
-kutegemeana na Umri, dawa uzitumiazo(kama unatumia), uwezekano wa magonjwa mengine ya mfumo wa damu..yanaweza pia kusababisha.
Ni vyema kufika hospitali mapema kujua hasa shida iko wapi.