SoC04 Kuboresha huduma ya afya kwa mama na mtoto

SoC04 Kuboresha huduma ya afya kwa mama na mtoto

Tanzania Tuitakayo competition threads

Albert Wilson Albert

Senior Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
191
Reaction score
226
TANZANIA TUITAKAYO

Niingie katika lengo la andiko langu moja kwa moja;

Katika jamii yetu na Taifa kwa Ujumla, kumekuwepo Malalamiko mengi juu ya Akina Mama Wajawazito pindi waendapo kujifungua na Ikaonekana wafanyiwe Operation.

Kutokana na hilo hujikuta njia panda kwa Kukosa pesa na Mahitaji muhimu kwa wakati huo.

Katika Tanzania Tuitakayo nilikuwa natoa mchango wangu kama ifuatavyo ili Kuwaokoa Wajawazito wote Nchini katika kipindi cha kujifungua ili Waepukane na Gharama, serikali ifanye yafuatayo.

Katika afya serikali ianzishe midahalo mashuleni na sehemu za kazi katika nyanja ya mahusiano na kazi ili miaka ijayo kuwe na kizazi chenye afya ya akili kwa kutambua wajibu wao na jinsi ya kuwa karibu ya wenye uhitaji katika jamii.

Lakini pia kwa kila Mwanachama wa NSSF na PSSSF wanaofanya kazi Serikalini, Jeshini, Viwandani na Sehemu yoyote ambayo kuna hiyo michango tajwa hapo juu.

Serikali ikate sh. 1,000 kila Mwezi kwa Wanachama wote ambapo kuna uwezekano wa kupata zaidi ya Bilioni 1 kwa Mwezi, Pesa hiyo ipelekwe kwenye Hospital zote Nchini ili Kina Mama WAJAWAZITO kipindi waendapo Kujifungua au kama ikitokea Wafanyiwe Operation basi hudumu zote wafanyiwe bure na gharama za huduma ambazo zinatakiwa kwao kuwepo wakala wa kujaza taarifa na kuzituma Wizara ya Afya pesa itumwe kwenye account ya Kituo cha afya kilichotoa hudumu kwa Mlengwa.

Hili linawezekana kama utaundwa mfumo ambao utachukua kiasi husika moja kwa moja na kuingia kwenye Account ya Wizara ya Afya kitengo cha Huduma kwa Mama Wajawazito tu na iwe endelevu.

Hii itaokoa wengi na kupata Kizazi endelevu chenye Afya njema na Ari ya Kujituma kwa maendeleo ya Nchi na Taifa kwa ujumla Maana bila Uzazi Salama hakuna Kizazi cha kuja kulijenga Taifa kwa baadae.

Mimi ni
FILMON WILSON ALBERT
0768941657
awilsonalbert@gmail.com
 
Upvote 0
Back
Top Bottom