SoC04 Kuboresha huduma ya Afya Vijijini

SoC04 Kuboresha huduma ya Afya Vijijini

Tanzania Tuitakayo competition threads

kungwe

New Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
2
Reaction score
3
Miaka 63 ya uhuru wa Tanzania kumekua na juhudi mbali mbali kama nchi na wadau mbali mbali kufikisha huduma za afya mijini na vijijini. ikiwa ni pamoja kuongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma pia kuongeza idadi ya watumishi wa afya. Juhudi zote hizo za serikali lakini bado kuna maeneo kama nchi hatujafanikiwa sana.

Changamoto kwa kiasi kikubwa wananchi wa vijijini wamekuwa wakipata huduma ya matibabu bila vipimo zaidi ya malaria,swali ni je malaria ndio ugonjwa pekee vijijni?
Taarifa iliyotolewa na wizara ya afya mwaka 2023 zaidi ya 33% watu waliopata huduma za kiafya nchini walipata katika ngazi ya zahanati, wakati taarifa hiyo ikisema watu hao wamepata huduma katika ngazi ya zahanati pasipo kusema ubora wa huduma katika vituo hivyo.
Hali ya kusuasua huduma katika zahanati za vijijini imetokana na sababu zifuatavyo​
  1. Idadi ya watumishi vituoni​
  2. Aina ya watumishi wanaotoa huduma​
  3. upungu wa baadhi huduma za msingi​
Katika makala hii nitagusia huduma ya afya katika zahanati vijijini upande wa vipimo, ikumbukwe kuwa vijijini zahanati hizi za serikali ndio msaada pekee walionao na changamoto za huduma za afya vijijini ni nyingi sana naweza kuandika kitabu kwa kuzielezea

Idadi ya watumishi afya katika zahanati vijijini inatia huruma kwa wanoapewa huduma pia na watoa huduma, idadi kubwa ya zahanati zina mtumishi mmoja au wawili. Kwa muhjibu wa taarifa ya serikali ya mwaka 2018 Tanzania ilikuwa na jumla ya zahanati 4900 ikiwa na watumishi 28,352 watumishi wanotakiwa ni 94,995 upungufu ni 66,643 sawa na 70% Kwa muhujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 zaidi ya watu 39,262,484 wanaishi vijijini hiyo ni sawa na 65.6% ya wakazi wote Tanzania wanaishi vijijini.

Kwa takwimu zisizo rasimi( nimefanya mwenyewe katika halimashauri kumi nilizotembelea vijijini mikoa tofauti) zaidi ya 90+% ya zahanati vijijini hazina huduma ya maabara na wataalmu wa maabara hiyo ni kumaanisha zaidi ya watu milioni 39.2 wanatibiwa bila kupata huduma ya vipimo hiyo ni hatari kwa afya zao, hatari kwa uchumi wetu kwakua inaongeza matumizi mabaya ya dawa pia inaongea usugu wa vimelea kwa matumizi holela ya dawa
UTATUZI
Utatuzi wa changamoto hiyo ni ujenzi wa maabara na kuajili wataalamu kwa awamu kwa miaka kumi shida hiyo itakuwa imepungua kama sio kuisha kabisa kama ifuatavyo
ujenzi wa maabara unategemea huduma kama MAJI NA UMEME
NISHATI UMEME: Kwa taarifa ya REA na serikali ifikapo mwaka 2025 zaidi ya 90+% ya vijiji na vitongoji vitakuwa vimefikiwa na huduma ya umeme kwa sasa tutaanza na vijiji ambavyo tayari vina huduma hiyo

MAJI YA UHAKIKA: Taarifa ya wizara ya maji na umwagiliaji pamoja na ripoti ya kituo cha takwimu Tanzania ya mwaka 2022 huduma ya maji vijijini imefikia 74% tutaaza na vijiji vilivyofikiwa na huduma hiyo ya maji.

kwa upande wa ujenzi wa miundombinu ya maabara utekelezaji utagawinyika kwa awamu kama ifutavyo

KUNDI LA KWANZA: Baadhi ya zahanati zilizojengwa kuna vyumba vilikuwa mahususi kwa ajili ya maabara, isivyobahati havijatumika kulingana na malengo. Ni muda sasa wa kuvitumia ambapo marekebisho yake hayahitaji pesa nyingi zaidi. wadau, wananchi pamoja na serikali wakishirikiana vizuri katika kundi hili la kwanza utekelezaji wake unaweza chukua mwaka mmoja hadi miwili tatizo la miundombinu litakuwa limekwisha.

KUNDI LA PILI: Hili ni kundi la zahanati ambalo katika ujenzi wa awali hapakuwa na chumba kwa ajili ya maabara lakini kuna vyumba vingi ambavyo havitumiki na vinaweza kubadirishiwa matumizi na kuwa chumba ya maabara, hapa pia utekelezaji wake unaweza kuwa kuanzia mwaka mmoja hadi mitatu changamoto inakuwa imeisha.wadau wa afya, wananchi pia na serikali wakishirikiana vizuri
KUNDI LA TATU Ni lile ambalo katika ujenzi wa zahanati hapakuwa na mpango wa maabara lakini pia vyumba vya huduma ni vichache kwa maana ya kundi hili litahitaji kupewa muda kidogo wa kutimiza kwakua litahitaji kujenga jengo lingine la maabara,wadau, wananchi pamoja na serikali wanaweza kutimiza hili ndani ya miaka miwili hadi mitano
Vifaa vya maabara ..kwa matumizi ya zahanati maabara zake zinakuwa na vifaa vichache kwa ajili ya upimaji vipimo ya kawaida vifaa vya vyake ni

  • Binocular microscope bei ni Tsh 1,324,400
  • Centrifuge machine bei Tsh 464301
  • Stool container (kopo za kuchukulia haja kubwa) 212 hizi kituo kinaweza kuagiza kulingana na idadi ya wagonjwa wake kwa miezi miwili miwili
  • Urine container (kopo za haja ndogo) @ 225 hizi pia unaweza kuagiza kulingana na matumizi
  • Haemochromax kwa ajiri ya kupima wingi wa damu hizi 90+% ya zahanati tayari zinapatikana
  • ACCUCHECK glucose @16122 kwa ajili ya kupima sukari kwenye damu
Bei za vifaa hivyo ni kwa muhujibu wa bei bohari ya dawa(MSD) ya mwaka 2023/24 zinaweza kubadilika kulingana na mwaka wa manunuzi au kama bidhaa ikikosekana MSD ikalazimika kuagiza kwa mzabuni teule japo mabadiriko ya bei hayawezi kuwa makubwa sana. Vifaa vyote hivyo vinapatikana bohari ya dawa MSD

Watumishi== hadi mwaka 2018 Tanzania ilikuwa na jumla ya zahanati 4900 ikiwa na jumla ya wataalamu wa maabara 909. Mwaka 2019 zahanati 7042, mwaka 2020 zahanati 7163, mwaka 2021 zahanati 7189, mwaka 2022 zahanati 7447, 2023 zahanati 7804 amabyo ni sawa wastani wa zahanati 190 kwa mwaka

Kila mwaka Tanzania inapata wahitimu wa taaluma ya maabara katika ngazi ya astashahada na sitashahada Zaidi ya 4161, hii ni kumaamisha kama serikali ikitoa ajira ya wataalamu wa maabara kila mwaka wataalamu 1000 ikiwa ni sawa na wataalamu wa makadilio vituo vipya 190 jumlisha watalaamu 810 kuziba upungufu uliopo itachukua miaka saba hadi kumi kupunguza kama sio kumaliza tatizo hili Tanzania hiyo ni kama kasi ya kuongezeka zahanati itabaki katika wastani huo wa ukuaji
 
Upvote 6
Back
Top Bottom