UTANGULIZI
HUDUMA YA AFYA YA AWALI; Ni mtazamo wa jamii nzima ambao unalenga katika kuhakikisha huduma za afya zilizo bora zinatolewa na kwa jamii nzima kwa usawa na kujali mahitaji ya wanajamii nzima. Hii inajikita katika utoaji wa huduma za kafya za kibinafsi zinazotolewa kwa mara ya kwanza kwa kila mwanajamii . Au kwa maana nyingine tunaweza kusema kuwa ni utoaji wa huduma za afya kwa kaya zenye kipato cha chini. Pia tunaweza iangalia hii HUDUMA YA AFYA YA AWALI kwamba imelenga katika maendeleo ya binadamu kiuchumi, kijamii na kiserikari na sio tu utoaji wa huduma za kiafya.
Mwaka 1978 kwa mara ya kwanza viongozi kutoka nchi mbalimbali Duniani walikutana Alma-Ata, Kazakhstan, kwaajili ya semina ambayo ililenga kukuza na kufanikisha (primary health care) ulimwenguni kwote ambao uliitwa ( Declaration of Alma Ata ). Miaka 40 badae walikutana tena Kazakhstan ikiwa ni mjumuisho wa viongozi , mshirika binafsi, wawakilishi wa serikali pamoja na asasi za kiraia. Global Conference On Primary Health Care, ulifanyika Astana Oktoba 2018 na ulijulikana kama ( Declaration of Astana). Ililenga kufanikisha malengo haya;
i.) Kufanya uchunguzi wa kisiasa kwa afya katika sekta zote
ii.) Kujenga huduma endelevu za afya ya msingi iliyochukuliwa muktadha wa ndani.
iii.) Kumwezesha mtu binafsi na jamii kwa ujumla.
iv.) Kuunga mkono wadau kwa sera za kitaifa.
NINI UMUHIMU WA HUDUMA YA AFYA YA AWALI?
Huduma ya afya ya awali ni muhimu kwasababu ni huduma inayo msaidia mgonjwa kupata huduma mapema na kumuweka katita hali ambayo ni salama endapo atahitaji kupata rufaa ya matibabu. Pia mi muhimu kwasababu inasaidia kugundua kwa halaka viathiri vya afya katika jamii ukilinganisha na msaada unaotolewa na mahospitali makubwa katika ugunduzi uo. Ni muhimu kwa sababu ni huduma iliyo karibu na jamii kwa ujumla.
UMUHIMU WA HUDUMA YA AFYA YA AWALI UMELENGA KATIKA VIPENGELE VITATU;
I. Kukidhi mahitaji ya afya ya watu katika yao yote.
II. Kushugulikia kwa upana viathiri afya (health dertaminants) kupitia sekta mbalimbali.
III. Kuwawezesha watu binafsi, familia, na jamii kuchukua jukumu la afya zao wenyewe.
NINI CHANGAMOTO KATIKA KUFANIKISHA PRIMARY HEALTH CARE?
Changamoto kubwa inaweza kuwa ni uchache wa wafanya kazi na vitendea kazi vya kutosha katika vituo vya afya. Kutokuwepo kwa wafanyakazi walio bobea pia inarudisha nyuma kuendelea na kukua kwa (Primary Health Care), pia miundombinu hafifu yakufanyia kazi ni changamoto.
NINI KIFANYIKE KUBORESHA MFUMO WA HUDUMA ZA AFYA ZA AWALI ( PRIMARY HEALTH CARE).
1. KUAJIRI WAFANYA KAZI WALIO BOBEA ZAIDI KWENYE VITUO VYA AFYA KULIKO KWENY HOSPITALI KUBWA.
Kama tunavyojua rasilimali watu ni kama moyo katika utoaji wa huduma za kiafya, hivyo idadi, umahiri, mgawanyo ni vitu vianavyo hitaji kuangaliwa. Ningependa kuishauri wizara ya ya afya kuajili madaktari, wauguzi, na wafanya kazi na wengine walio bobea zaidi katika vituo vya afya kwani ingesaidia katika kupunguza rufaa za matibabu ambazo zinamuweka mgonjwa katika hatari ya kupoteza maisha pia hii itapunguza vifo visivyo vya lazima. Kama vituo vya afya vitakuwa na wabobezi wa afya wagonjwa watapokea huduma nzuri na kupunguza vifo na kama rufaa itafanyika basi itamuweka mgonjwa hatari ndogo ya kupoteza maisha kwani atakuwa amepewa huduma ya kwanza iliyo bora.
2. KUWEPO KWA MUUNDO WA HUDUMA UNAOTOA KIPAUMBELE KWENYE HUDUMA YA AWALI ZAIDI.
Utoaji wa huduma ya msingi yaani inayoendelea, ya kina, iliyoratibiwa, na inayo wagusa watu katika vituo vya afya unapaswa kupewa kipaumbele zaidi kwa kuwategemeza katika Nyanja mbalimbali kama madawa, miundo mbinu. Mikakati inapaswa kuendelezwa ili kuhakikisha kwamba huduma za awali katika vituo vya afya ina uwezo wa kuchanganua matatizo yoteya kiafya yaliyopo na mapya katika jamii na kuwa na jukumu la usimamizi wa maendeleo ya mgonjwa.
3. KUWEPO KWA SERA MKAKATI KWENYE SEKTA MBALIMBALI( MULTISETORAL POLICES AND ACTION).
Afya na ustawi wa watu na jamii unatokana na muingiliano wa awali wa jamii, uchumi, mazingira na visababishi au viathiri vya afya, ambapo ndani ya hivi vitu tunakutana na uchafuzi wa mazingira, umaskini unaopelekea kutopata huduma sahihi za afya, ukosefu wa elimu, nakuwepo kwa matabaka. Hivyo ningependa kushauri sekta ya afya kujikita zaidi katika uchanganuzi wa sekta mbalimbali katika kuhakikisha inaboresha huduma ya afya ya awali.
4. KUWEPO KWA DHAMIRA YA KISIASA NA UONGOZI (POLITICAL COMMITMENT AND LEADERSHIP).
Kuwepo kwa dhamira ya siasa na uongozi katika sekta ya afya ni muhimu sana kwasababu mabadiliko ndipo yanapotegemea.hivyo basi ni ushauri wangu kwamba viongozi yawapasa kulichukulia swala hili kwa kuunda utendaji ndani yake, kwa mfano kupitia maadhimisho au tamko, kuongelea zaidi umuhimu wake, kutoa fedha za kukidhi sekta za afya na kujikita katika utekelezaji wa jitihada za kukuza primary health care. Katika uchanganuzi wa viathiri vya afya( health determinants) kijamii, kiuchumi, na kimazingira kupitia sera za sekta mbalimbali vinahitaji kuwepo kwa dhamira ya siasa na uongozi katikakufanikisha.
Pia ili watu na jamii nzima iweze kuwezeshwa kutoka kwenye majanga ya kiafya inabidi uongozi uchukue nafasi katika kufanikisha. Jamii kubwa ina hali mbaya ya afya ambayo inasababishwa na unyanyasaji eidha wa kijinsia, kiumri, hali za kiuchumi, kielimu, ulemavu au kidini.
5. KUWEPO KWA MFUMO WA KUBORESHA HUDUMA (SYSTEM FOR IMPROVING HEALTH CARE).
Ni ushauri wangu kwa serikari kuhakikisha kuwa kuna kuwepo mfumo unaoweza kuboresha huduma za afya. Kwasababu “The lancet global health commission on high quality health system” ulionyesha kuwa vifo katika nchi zinazoendelea vinasababishwa zaidi na ubora hafifu wa huduma za afya kuliko upatikanaji wa huduma hizo. Kama huduma nzuri na zenye viwango zitapatikana kwenye vituo vya afya itapelekea kupunguza vifo katika jamii.
HITIMISHO
Nipende kutoa wito kwa wizara husika kwamba huduma ya afya ya awali (Primary Health Care) inapaswa kuangaliwa na kutegemezwa sawa na huduma za afya za juu kwani vituo vya afya vikiboreshwa vitapunguza msongamano kaktika hospitali kubwa pia kutapungua vile vifo vinavyo sababishwa na ucheleweshwaji wa huduma za mgonjwa aliye pewa rufaa kwenda hospitali kubwa.
Nawasilisha.

Upvote
1