Superbrand
JF-Expert Member
- Apr 6, 2013
- 509
- 158
Kupitia ukuaji wa Teknolojia ya mawasiliano na Habari, Tanzania imeweza kuunda mifumo ya usimamizi wa Taarifa za wagonjwa.
Mifumo hii iliyoundwa bado kwa sasa imekuwa ina changamoto kubwa ambayo ni kuwa haisomani na kupelekea kutokuwa na Tija.
Mgonjwa anaenda hospitali ambapo tayari ashawahi kuenda lakini anahitajika kuwa na kadi ya usajili tena.
Mifumo hio inatakiwa kuboreshwa na kufanya taarifa za wagonjwa nchi nzima ziwe katika Data center moja, mwananchi akienda katika hospitali moja achukuliwe tu alama za vidole na utambuzi ufanyike wa kujua historia yake ya kimatibabu.
Mashine kama zile za usajili wa laini zinaweza kutumika kuchukulia taarifa za utambuzi hospitali na zikiwa zimeunganishwa katika kanzi data ya usajili wa laini.
Mtu akiweka alama yake ya kidole iwe imetosha kuchukua taarifa, sio kufika kila hospitali na kuulizwa taarifa zile zile ambazo zinacheleweshwa mgonjwa kutibiwa.
Asante sana.

Upvote
0