Technically,damu ni chafu muda wote.Na ndio maana tumeumbwa kuwa na damu.Kazi mojawapo ya damu ni kubeba na kusafirisha uchafu/takamwili(waste products) kutoka mahali zinapozalishwa na kuzipeleka mahali zinapotokea nje(excretion).
Si sahihi kusema kwamba septicemia,viraemia au parasitaemia ndio kuchafuka kwa damu;hayo ni maambukizi tu na hata mtu akitibiwa akapona bado damu inaendelea na ile kazi yake ya kubeba na kusafirisha uchafu unaozalishwa mwilini.
Si sahihi pia kusema mtu mwenye VVU au magonjwa mengine ya zinaa ndio damu yake imechafuka.Maana bado inakuwa inaendelea na jukumu lake lile lile la kubeba uchafu kama watu wengine.
Neno hili la kuchafuka kwa damu limekuwa likitumiwa vibaya,na kwa mtazamo wangu,limekuwa likitumika ktk kunyanyapaa watu waishio na VVU.Imekuwa ni kawaida kusikia watu wakisema "Nimepima nimekuta damu yangu ni safi!" hapo wakiwa na maana kwamba amekuta hana VVU.Na leo hii ni kawaida kusikia "Ah.. jamaa ameishachafuka damu huyo,kaa naye mbali" Hii sio sahihi;sisi sote damu yetu ni chafu,so log as bado inatekeleza jukumu lake la kubeba uchafu.