Watanzania wenzangu inabidi tuache Ushabiki na tuangalie mustakabali wa nchi yetu. Pengine tunashabikia bila kufahamu mambo haya. Kuipa kura CCM itakuwa ni 'grave mistake' kwa watanzania. Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo
- CCM ikiingia madarakani itakuwa ni kama imepewa go ahead na ufisadi, watafanya ufisadi kama kawaida na hata wapinzani wakipinga bado watakuwa na strong point kwamba kama CCM ni mafisadi mbona wananchi walitupa ridhaa ya kuongoza nchi? hakuna mtanzania hatakaye weza kujibu swali hilo.(swala la kuiba kura halitakuwepo hapo)
- Ishu za kagoda, meremeta, kiwira ndo zitakuwa zimezikwa rasmi HUTAZISIKIA TENA, na hata wapinzani wakitaka kuibua kashfa itakuwa ni ngumu kwa maana watawambia si mliwaeleza wananchi kuhusu ufisadi huo,kama ni kweli si wangewapa ridhaa ya kuongoza nchi, watasema siku zote wapinzani ni waongo
- Lowasa na wenzake watakuwa na nguvu kubwa sana ya kurudi serikalini na hata kugombea Uraisi. kwa kigezo cha kwamba kama kashfa zake zilikuwa za kweli mbona wananchi walimchagua tena kwa kishindo(Mtanzania uliye makini kumbuka maneno ya kikwete alipokuwa akimnadi lowasa,mramba)
- CCM watahakikisha wanaweka sheria ngumu mno kwa wapinzani kuhakikisha kwamba they will never ever try to challenge the ruling party CCM.