Kuchagua mawaziri kuwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa bunge la Katiba tunajifunza nini?


Hili la Jaji kuwa mwenyekitii ndoo kabisaaa uozoo...wajua majaji wote ni wateule wa Raisi huku wengi wao wakipewa kama fadhila, ukada na urafikii??
Kosa kubwa hata Rasimi hii imekosa sana misingi ya utawala na maadili yake. Yahitajikaa Katiba itakayojalii sana Maadili na Uongozi hasa upatikanaji wa viongozi kama Majaji, mawaziri, wakuu wa taasisi za umma, usimamizi wa mapato na matumizi ya umma, na rasilimali zetu.
 
mchakato ulipofikia haususiki tena - tumeshayavulia nguo.....
Wenzetu jirani zetu Kenya waliususa mchakato wa kwanza wakaanza upya. Sasa hivi pamoja na tatizo lao kubwa la ukabila wana moja ya KATIBA nzuri sana barani Africa.
 
Wapo Majaji wazuri tu nchi hii akina Robert Kisanga, Barnabas Samatta, etc., ambao wangeweza kulisimamia jambo hili bila bias yoyote kwa mtu wala kundi lolote.
 
Wapo Majaji wazuri tu nchi hii akina Robert Kisanga, Barnabas Samatta, etc., ambao wangeweza kulisimamia jambo hili bila bias yoyote kwa mtu wala kundi lolote.

Natumai hao uliowataja (Kisanga na Samatta) wajua watawala hawakuwafurahiaa kwa misimamo yao na kamwe hawawezi kuwashirikisha uongozi katika utungaji wa Katiba hii..
 

Hamy-D, naomba usome vizuri uzi wangu. Nilisema mtu ambaye ni waziri. Kificho ni spika wa baraza la wawakilishi nafasi ambayo inamfanya asimamie mhimili mwingine wa dola na siyo waziri. Sitta na Samia ni wajumbe wa baraza la Mawaziri kwa hiyo wako chini ya muhimili mmoja wa dola na wanakwenda kuongoza mhimili mwingine. Hilo ndilo lilikuwa suala langu
 
Watakwambia hili ni BUNGE MAALUM hivyo WAJUMBE wote walioko mle wana hadhi sawa ingawa tunawaona wanaitana kwa hadhi na vyeo vyao. Watakwambia pia kwamba Sheria ya Mabadiliko ya Katiba iko kimya juu ya hili.

Ni mambo kama haya ndio yanayotushangaza kuwa watu makini kama akina Tundu Lissu hawakuyaona haya hata walipopata fursa ya kuonana na Jakaya wetu ana kwa ana. Niliwaona juzi wakisifiana kwa kutengeneza KANUNI nzuri zitakazo liongoza bunge hili ambalo tayari limetekwa na CCM.


Historia haitawaacha watu hawa.
 

Teh teh teh nimecheka sana ulivyosema wataniambia kuwa hili ni bunge maalum. Hivi katika siku zote hizo baraza la mawaziri halitakutana? Je likikutana nani ataongoza vikao vya bunge maalum au watakuwa wanapeana zamu? Nadhani kama unavyosema kuna wakati inatakiwa tuwe makini kidogo na mambo tunayoyafanya.
 
Asante studioo, Samia hakupenda katiba mpya tangu akiwa makamu wa mwenyekiti wa bunge la katiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…