Kuchakachua........

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2008
Posts
5,457
Reaction score
963
Wajuzi wa lugha..naomba kufahamu neno KUCHAKACHUA linatokana na nini na maana yake ni nini.Miaka ya nyuma kulikuwa na bendi inapiga muziki kwa style ya "CHAKACHUA" - Je kuna uhusiano wowote na neno hili?
 
wos neno kuchakachua ni neno linalotokana na kitendo cha wafanya biashara ya mafuta
ya petroli kuchanganya mafuta ya petroli na mafuta ya taa ili waongeze quantity na faida....

mafuta ya taa bei yake ni nafuu kutokana na kodi ndogo....

sasa mitaani ndio mchezo wa kuchanganya mafuta unaitwa chakachua.....

hiyo bendi hata mimi nili wahi isikia but sidhani ....
 
Boss,
Je ni neno rasmi au ni lugha za mitaani maana nalisikia na kulisoma hata kwenye vyombo vya habari.
 
lilikuwa neno la mitaani...sasa lilipoingia bungeni ndio limekuwa rasmi...
 
Tatizo ni jinsi linavyotumika - unalisikia kila mahali.. mara kuchakachua wagombea, mara kuchakachua mafuta?Nilidhani kwamba kuchakachua ni
"adulteration" kwa lugha ya wenzetu .. au nakosea? na kama ndio, je inawezekana vipi kuchakachua wagombea wa ubunge au udiwani?
 

kuchakachua kwa maana ya kufoji....
au kutoa kisicho halisi,au kutumia mizengwe...
sasa kwenye wabunge wanaokuwa refered hapa ni wale
ambao hawakushinda kihalali lakini wamepitishwa...
mfano waliochapisha kadi feki,umenipata???????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…