Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Njia ya kuchanganya chanjo za Covid -19 kwa kutumia chapa mbalimbali za chanjo ya Covid kwa dozi ya kwanza na ya pili - inatoa kinga nzuri dhidi ya virusi vya janga hilo, utafiti wa Uingereza umebaini.
Majaribio yalitazama ufanisi wa dozi mbili za Pfizer, AstraZeneca na Mchanganyiko wote ulifanya kazi vizuri, ikitoa kinga ya mwili. Ujuzi huu unaweza kupokea mazingira ya chanjo inayotolewa, wanasema wataalamu.
Matokeo ya majaribio yanaonesha kuwa watu ambao wamepata dozi mbili za AstraZeneca wangeweza kuwa na kinga yenye nguvu kama wangepatiwa chanjo tofauti kama nyongeza.
Naibu Afisa Mkuu wa kitabibu nchini Uingereza, Prof Jonathan Van-Tam, amesema hakukuwa na sababu ya kubadili dozi za sasa za chanjo zinazoonesha mafanikio nchini humo, zikiwa zinapatikana vyema na kuokoa maisha.
Lakini anasema inaweza kuwa kitu cha kuangalia katika siku zijazo: "Kuchanganya dozi kunaweza kutupa mabadiliko zaidi kwa programu ya nyongeza, wakati pia ikisaidia nchi ambazo zinaendelea zaidi na utoaji wao wa chanjo, na ambao wanaweza kuwa na shida za usambazaji . "
Baadhi ya nchi tayari zinaztumia dozi mchanganyiko. Uhispania na Ujerumani wanatumia Pfizer au Mordena ya mRNA kama dozi ya pili kwa vijana ambao tayari walishapata dozi ya chanjo ya AstraZeneca, kutokana athari za kuganda kwa damu zaidi kuliko ufanisi.
BBC Swahili