Kuchanganya lugha zaidi ya moja ni usomi

Kuchanganya lugha zaidi ya moja ni usomi

Ni usomi eeee?

kwa nini unafikiri hivyo?
 
1. Iko otomatiki kama unazifahamu zote
2. Kujisikia, dalili kuwa biya zimekolea, ....
3. Usomi uliotukuka
 
Sifikirii kama ni usomi bali ni kutaka uonekane msomi. Hii tabia kusema kweli inanikera hasa kwa watunga sheria wetu.

Kuchanganya lugha mara nyingi inatokea pale Mswahili anapozungumza Kiswahili na Waswahili wenzake, mara anatometomea maneno ya Kiingereza (tena kibovu au bombastic words) aonekane msomi. Kwa nini mtu huyu huyu akizungumza na Waingereza au Wazungu wengine hachanganyi na Kiswahili chake?
 
Nadhani wapo baadhi ya watu wanaoshikilia hiyo dhana. Na pia wapo wale wanaohusisha Kiingereza na ustaarabu na hadhi fulani ya kimaisha.

Ni moja ya athari za kasumba za ukoloni.
 
Nikiongea kimakua na Kiswahili nikiwa kijijini hakuna anayetahamaki, ikitokea nikichanganya Kiswahili na English baadhi ya wadau wanaanza kuzozomoka. Hii kitu inatokea na nahisi ni ngumu kujizuia
 
Back
Top Bottom