Pendaelli
JF-Expert Member
- Feb 13, 2014
- 11,050
- 31,412
Salamu kwa wote na heri za maadhimisho ya kumbukumbu ya muungano wetu.
Tuna kila sababu ya kuwapongeza waasisi wetu kwa kuwa na fikra chanya za kutaka kuungana na hatimaye ikawa hivyo.
Umoja, undugu, mshikamano kwa kiasi kikubwa imekuwa sababu ya kupelekea maendeleo ya moja kwa moja kwa wale wanaoungana iwe ni taifa au kikundi au mtu mmoja mmoja.
Lakini kama ilivyo ada ya mwanadamu asivyo mkamilifu na asiyejua kwa ukamilifu lililo mbele yake, kunaweza kukawa na error zinazoweza kujitokeza na kupelekea kuona ile sababu ya kuungana haipo tena, na suluhu pekee ni kuvunja au kusimamisha kwa muda huo muungano.
Hapa kwetu wakati ule mataifa haya yalipoungana lilifanyika tunaweza kusema tendo la Kiibada la kuchanganya udongo wa mataifa haya.
Kitendo kile tunaweza kusema au kuona ni cha kawaida lakini kimantiki kina maana kubwa sana na kiasi inaweza kuleta gharama kubwa iwapo itafanyika kinyume chake.
Siku ikitokea inatakiwa muungano usitishwe, itawezekana je kuutenganisha ule udogo uliochanganywa?
Wajuzi wa mambo ya kiroho labda wanaweza kutujuza labda kuna ibada inayoweza kutenganisha automatically.
View attachment 2599824