Hapa ndio pale elimu ya uraia na wapiga kura ya kweli inapohitajika. Maskini wadanganyika bila kujua kwanini wanachangia, watachangia kwa nguvu zote. Halafu zile watakazochangia zitarudi kwa wachache wao wenye kelele kwa njia ya Kofia, na T-shirt bila kugundua hawajakamilishiwa cha kuvaa chini na hivyo wapo utupu! Na watajisifu kwamba wamekula pilau za bure na hivyo wapo radhi kuwapa kura. Mwaka mmoja baadae watalia kilio cha mbwa mdomo juu maisha magumu!
Tanzania...Tanzania...kwa nini wanakufanya hivi?