Kuchangia gharama za uandikishaji zoezi la kuboresha daftari la wapiga kura serikali za mitaa ipo kisheria?

Majitha

Member
Joined
Jan 4, 2016
Posts
17
Reaction score
8
Habari wananzengo,

Tumesambaziwa barua na Chama cha Mapinduzi kutuomba kuchangia kuboresha zoezi la kulipa kura, lakini mie nahisi harufu na rushwa na kupigwa maana daftari ya kupiga kura inaboreshwa na Tume, iweje chama ndiyo kituletee barua.

Naomba kusaidiwa. OR TAMISEMI

 
barua haina hata muhuri ,huo ni upigaji wa wazi kabisa
 
Tume inaboresha Daftari la Kudumu la Wapiga kura kwa ajili ya Uchuguzi Mkuu.

TAMISEMI inahusika na uandikishaji wa Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Hakuna chama kinahusika moja kwa moja na jukumu la Wapiga kura, isipokuwa vyama ni wadau tu.
 
Kama ni kweli basi hii nchi ishaharibika,na kauli ya kibaki inazidi kudhihirika
 
Haya ndio makosa tungeona mtu amepelekwa mahakamani au amewajibishwa na taasisi yake, lakini hata siku moja ni ngumu. Hali yetu ya demokrasia ndio hiyo
 
Vyama vya kisiasa hushiriki Kwa kuweka mawakala wakati wa uandikishaji na siku ya uchaguzi. Mawakala hao hulipwa na chama au hujitolea hivyo kama unao wape kama huna acha waendelee na utaratibu wao.
 
Hawahusiki Moja Kwa Moja lakini huweka mawakala ambao chama kinatakiwa kuona namna ya kuwezesha chakula au posho
 
Sisi wenzako tumekwisha changa siku nyingi, mambo ya chama usihoji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…