Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Nchi ina vipaombele lakini suala la mafao linapaswa kuwa kipaombele Cha Kwanza. Nipo na watu waliostaafu utumishi wa Umma wengi wakiwa walimu na wahudumu wa afya, Wana maisha magumu.
Tafakari walikua na mshahara mdogo kwa maisha yao yote ya utumishi, wakafanya kazi kwa kujibana wasomeshe watoto. Leo wamestaafu hawana
-Hawana mshahara
Hawa watu wamehama wamerejea kijijini, wengine wamebaki mjini na watoto wao bado awajapata ajira..inaumiza sana.
Kibaya zaidi wanajitahidi kutumia kidogo walichonacho kufuatilia, kila siku wanapigwa Tarehe na wanaowapiga Tarehe kwa kuwadanganya wengi wao ni watoto wao yaani vijana waliojiriwa hivi karibuni. Unakutana na mzee amebaki kuwalaani wafanyakazi wa mifuko ya jamii hadi unajiuliza tatizo ni mifuko au tatizo ni kipaumbele Cha serikali. Hivi kweli viongozi waandamizi awajui nani anastaafu lini?
Lakini kibaya zaidi, wakubwa wote mara tu wanapostaafu wanaingiziwa chao. Hakuna mbunge, mkurugenzi, DC, Katibu tawala na wakuu wa Idara anayestaafu akakaa mwaka bila kulipwa mafao....je Hawa watumishi wa chini wanatofauti gani na hao wakubwa zao?
Tuwaonee huruma Hawa maana stress na umri zinawaondoa mapema bila hata kupata mafao yao matokeo yake watoto wanapigania mafao na wengine kufarakana Kama siyo kuuwana.
WALIPENI HAKI YAO, HATI MKIWALIPA FEDHA WALIZOKUWA WANAKATWA ITASAIDIA WAKATI MNATAFUTA FEDHA ZA MWAJIRI NA MFUKO HUSIKA.
MWENYENZI MUNGU ALAINISHE MIYOYO YENU MKAWATAZAME HAWA WAZAZI WENU KWA JICHO LA HURUMA

- Pensheni kwa maana mafao ya mkupuo
- Hawana malipo ya mwezi