Mkuu maji yanatoka point A kwenda point B kwa kufuata njia ambayo tunaita mkondo. Sasa kuna mikondo ya aina mbili,mkondo wa kulazimisha na mkondo usio wa kulazimisha.
Mkondo wa kulazimisha ni pale unapotaka maji yatoke point A ambayo ipo chini au sawia na point B. Hapo inabidi utumie kifaa kama pampu.
Mkondo usio wa kulazimisha ni pale maji yanapotoka point A ambayo ipo juu kwenda point B ambayo ipo chini. Hapa huitaji pampu. Sasa basi ili wazo lako litimie hakikisha unatengeneza mkondo wa maji katika mfumo wako wa nyumba.