Kuchomekea kadeti ni ushamba?

Actually nguo nzuri zote huwapendeza watu warefu.

Nguo pekee zinazowapendeza watu wafupi ni msuli na kanzu.
Kwa kifupi kitambi kinaondoa kabisa muonekano mzuri kwa mwanamme.......si kwa mfupi wala mrefu
 


Mimi sitaki kuamini usemacho.Huyo anaesema kadeti haichomekewi ni nani? Hata ukiacha hiyo nadharia ya "Be you", bado kwenye ulimwengu wa fashen suruali hii inakamata sana.Mwenyew umepost picha hapo za hao watanashati.

Usikute umezengukwa na wale watu wa kuvaa nguo za wapuliza tarumbeta. Siku hizi google tu utapata kujua nini kina trend.
 
Jamani mimi ni mrefu wa wastani, yani ni mrefu lakini siyo super tall.Kinachonikera ni umbo la kubinuka. Yani sinyooki, hivyo, hata kama sina kitambi kitumbo kinafyatuka na kuonekana kama kitambi.Hali hii inanikera sana.

Kila nikikipigia mazoezi wapi.Kinaniharibia pozi la kuulamba sana, shenzy type.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…