Kuchukua mkopo bank

Benno

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2009
Posts
332
Reaction score
51
Niliwahi chukua mkopo bank moja nitaitaja baadaye,
tukakubaliana wakate makato tare 30 ya kila mwezi kasoro february,
cha kushangaza banki hiyo imebadili tarehe ya kukata na kuweka tarehe 23. Na 24 ya kila mwezi,

sasa mshahara ukichelewa tuu kuingia wanakata kilichopo hata kama umeweka kwa matumizi ya familia na unajikuta unadhalilishwa pasipo sababu.

1. Nilishawahi tumiwa pesa na boss wangu toka nje nimpe mke wake hospitali, nimetoka na mwanae mpaka bank nakuta pesa imekatwa.


2. Nilikabidhiwa pesa ninunue baiskeli ya mlemavu siku nikaweka bank ili nisiitumie siku ametoka hospitali nimeenda naye bank nakuta hakuna kitu, nilipojaribu kumwelezea aliangua kilio na nikafedheheka sana.

Nimewaeleza wahusika naona napigwa danadana


naomba msaada wa kisheria nifanyeje?
 
Izi bank ziko very dis organised!yashawai kunikuta hayo mara wasikate ela then baadae wanakata za miezi 2 mara moja
 
Hizo ndiyo benki za kibongo wanashindwa ku honor contract waliyoingia na mteja. Kama una hiyo contract inayosema wanatakiwa wakate tarehe 30 ya kila mwezi, nenda nayo kwa meneja na umwambie akishindwa then tafuta msaada wa kisheria. Hata kama wanakudai hawatakiwi waende kinyume na makubaliano yenu.
 
Mbona unaificha hiyo bank,huu ndio uwoga na unafiki.
 
taja tu bank gani mkuu manake nina mpango wa kwenda kukupa sasa hivi nisije angukia pua.
 
CRBD bank ndio wenye utaratibu huo. Kwa kweli wanakera sana wateja!
 
Izi bank ziko very dis organised!yashawai kunikuta hayo mara wasikate ela then baadae wanakata za miezi 2 mara moja

I am not condoning this disorganization in Tz Banks! BUT Mkuu Njowepo sasa kwa nini hukuwapigia au kwenda kuwaona pale ulipogundua kuwa hawakuchukua ule mwezi wa kwanza??you should have all time access to assess your account all the time mkuu.
 
Nilikimbia hizi bank nika enda hizo zinazojiita standard nikadhani kuna unafuu kumbe wanakubembeleza wakati wa kuchukua tuu. Wanakuomba uchukue mpaka unajisikia kero.
 
wakati wanakupiga danadana na unashughulikia swala hilo hakuna sababu ya kuendelea kufadhaika!

Banks ziko nyingi that unaweza kuwa na account nyingine ambapo hata mshahara ukiingia unaweza kuuhamisha au kuitumia kuweka akiba zako na kwa maswala megine kama hayo yalokusibu
 
Barclays ndio wezi wa kutupa ukichukua 1M utalipa 2.5m na deni lao haliishi ikipita tar 25 muajiri hajaweka wanakata 165 000 eti penalti na ukitaka benki ingine inunue mkopo wako wanapiga penalty sh laki 9 wakati haipo ktk mkataba.benki za bongo hazipo kumsaidia mwananchi zipo kwa ajili ya mafisadi tuu
 
Ndio adha ya mikopo somtimes lakini i guess ina depend na benki
 
Halafu mbona hasemi ni benki gani alichukua huo mkopo labda kuna watu wako huko wangemsaidia zaidi
 
Halafu mbona hasemi ni benki gani alichukua huo mkopo labda kuna watu wako huko wangemsaidia zaidi

I wonder! Sioni mantiki ya kushindwa kutaja jina.yeye anataka kusaidiwa but anashindwa kusaidia watu wengine ambao bila kujua watanasa kwenye mtego wa hiyo bank.huu ndio ubinafsi wa kibongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…