Neno hili nadhani linatokana na neno afanaleikh. Kwa kweli sifahamu maana ya neno afanaleikh.
Kudadeki leo limekuwa neno la kuonyesha mshangao au hamaki.
Zaidi hutumiwa na vijana
Kwa kesi ya hili nadhani linaendelea kuwa tusi, sababu hapa linatumika tu pale ambapo mzungumzaji yupo kwenye mazingira ambayo anahisi hataweza kutumia neno lile la mwanzo
Wachagga (wa Marangu) wakishangaa wanaweza kutumia neno 'mbula' ambayo ni tusi ila kutokana na mazingira wanaweza kutumia 'mbura' ambayo haina hata maana.