Taarifa zote ziungwe na namba za simu, haiwezi mpaka leo bado hatujaweza kuunga hizo taarifa na mifumo ikawa ama inasoma au ukawa mmoja wenye level tofauti za access kulingana na idara.
- Cheti cha kuzaliwa, hapa ni lazima wakusanya taarifa za wazazi wote wawili, zote.
- Kitambulisho cha mpiga kura, hapa pia wanakusanya taarifa zote za mhusika ambazo zitalinganisha na hapo juu kimfumo! Mawasiliano lazima yawepo.
- NIDA, hii ni lazima wachukue taarifa za kutosha kabisa, ambapo ulinganifu utafanywa na hivyo vilivyotangulia...hapa ni lazima iwe kitambulisho chenye sim/chip, kibebe mpaka taarifa za blood group, rangi ya macho, nywele, urefu, disability, next of kin, wazazi wote wawili, watoto, mwenza, level ya elimu, ajira, TIN, etc.
- Pasi ya kusafiria, inapata taarifa zote kutoka zilizotangulia juu pote, iwe ni suala la kuomba, weka finger print, kitu unaipata ndani ya masaa 24.
- Leseni ya udereva, hii pia iwe ni ya kupakuliwa kutoka kwenye taarifa zilizopo, kwenye display ioneshe na blood group.
Usajili wa vingine vyote ujikite kwenye kupata taarifa kwenye hivyo vitambulisho, kadiri maboresho yanavyotakiwa, kuna idara zipewe uwezo wa ku-update(bila kufuta taarifa zilizokwisha tangulia, ioneshe nani ameongeza taarifa pia) profile ya mhusika, iwe Hospitali, Polisi na Mahakama, Mamlaka ya vyuo na Shule.
Wanawezaje kupata namba kutuambia habari za utapeli na shughuli za kizimkazi washindwe kuunga taarifa zote?
- Number plate ikishakuwa scanned, itume ujumbe moja kwa moja kwa namba sajiliwa kwa taarifa zaidi!