Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania kwa mujibu wa katiba ya nchi,
Ni vizuri sana kuambiana ukweli kama wadau wa siasa na waTanzania kwa ujumla, kwamba eti kuna mabadiliko ya sheria za uchaguzi au katiba mpya sijui next week au next month taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu october, huo ni utapeli wa kisiasa na ni uongo mtupu. Hanuna mabadiliko yoyote kwa namna yote ile.
Vyama vya siasa makini,
mathalani CCM tayari wameshaamua na kumuidhinisha mgombea urais wa chama chao tayari kama sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Tanzania october mwaka huu2025. Jambo hilo likimaanisha kwamba wamejipanga vizuri sana mapema kwaajili ya uchaguzi huo, na kujizatiti kushinda kwa kishindo..
Kuchukua muda mrefu kudanganya wananchi eti hapatakua na uchaguzi mpaka mabadiliko ya sheria za uchaguzi yafanyike, ni kuhadaa wananchi mchana kweupe na kujidanganya kisiasa.
Badala ya kujiandaa na uchaguzi mkuu, mnahangaika kuandaa movements ambazo hazina maana yoyote kwa wananchi, zaidi sana zinawadidimiza na kuwadhoofisha wenyewe na vyama vyenu kwa ujumla.
Mabadiliko ya sheria za uchaguzi na tume huru ya uchaguzi yalishafanyika, na hakuna mabadiliko mengine yoyote yatafanyika kuelekea uchaguzi mkuu wa october2025.
Hakuna haja kudanganya wananchi.
Uchaguzi wa serikali za mitaa mlihamasisha watu wasiende kujiandikisha kupiga kura, halafu wakati wa uchaguzi mkaanza kulalama ati wagombea wameenguliwa na eti siju kura zimeibiwa?
Wanaruhusiwaje kugombea uongozi watu ambao hawajajiandikisha kupiga kura na wasio timiza vigezo na sifa za kikatiba? Na halafu sasa, mnaibiwaje kura wakati hamkujiandikisha kupiga kura na hamkupiga kura? hivyo si visingizio vya uongo ndugu zangu?
Na mnapingaje matokeo ya kura za wananchi waliopiga kura, hali ya kua ninyi hamkupiga kura wala hamkujiandikisha?
naona mnaendeleza yale yale mliokua mnajidanganya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kuelekea uchaguzi mkuu wa october.
Dhana potofu na mayowe ya kuibiwa kura, kususia uchaguzi au maandamano haramu ya kuleta vurugu,
hayatazuia wananchi wa Tanzania wenye sifa na vigezo vya kikatiba kushiriki zoezi la kupiga kura uchaguzi mkuu.
Ni ngumu kushindana na kuishinda CCM iliyojipanga mapema kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
Na mkiendelea kuzubaa na kumangamanga na blind movements, retreats, workshops na semina za kula bata kwenye mahoteli mbalimbali mjini, hamtaambulia hata diwani moja achilia mbali ubunge na urais ambao mtakua mnausikilizia kwenye radio na televisheni tu.
Una maoni gani?
Mungu Ibariki Tanzania