CAMARADERIE
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,419
- 1,923
Jana nikiwa kaunta ulizuka mjadala kuhusu mdau mwenzetu na ndoa yake. Kuna waliodai kuwa mkewe ana maringo sana na wengine wakidai mume anamdekeza sana. Binafsi sikuchangia kwa kuwa haya maneno yalinichanganya na wanywaji wale hawakunisaidia kuelewa japo sikuwa nimelewa. Nini tofauti ya hizi hali na madhara yake?