Kudhibiti mapato ya taifa

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,106
Reaction score
12,916
Kutokana na kukua kwa tekinolojia.Imefika wakati kwa taifa letu tutengeneze mfumo maalum wa kuangalia tumepata nini kwa kila siku na saa ngapi pato limeingia na pato hilo limetokana na kitu gani na ni sehemu gani hasa kijiografia.

Kila mwananchi awe ana access ya kuingia kwenye mfumo huo na kujua nini kinachoendelea katika kata, tarafa, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla, pia kama kuna fungu lolote limetoka nje tuweze kuliona.

Vile vile katika mfumo huo kutakuwa na repoti ya matumizi ambayo itaambatana na mfumo picha wa kazi iliyofanyika au kifaa kilichotumika na sehemu gani na wananchi watakuwa wana toa maoni na kugonga like .

Pia watumishi wote wa serikali tuwaone kwa picha zao na kiasi wanacholipwa na kazi wanazofanya sambamba na kodi wanazokatwa.(kama hii unaona ni siri kazi ya serikali haikufai ondoka). Pamoja na mawazo mengine ambayo mnaona yanafaa kuwemo.

NB:
Hii itawapa nguvu wananchi ni nini waamue mfano posho za wabunge fungu litoke wapi? Magari yao je? Ni muhimu kununuliwa gari.maoni watatoa wanachi kura zikipungua hakifanyiki kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…