๐Š๐ฎ๐๐ก๐ข๐›๐ข๐ญ๐ข ๐ฉ๐ซ๐ž๐ฌ๐ก๐š: ๐‰๐ž, ๐ง๐ข ๐ฅ๐š๐ณ๐ข๐ฆ๐š ๐ง๐ข๐ฐ๐ž ๐ง๐š ๐ค๐ข๐ฉ๐ข๐ฆ๐จ ๐œ๐ก๐š ๐ฉ๐ซ๐ž๐ฌ๐ก๐š ๐ง๐ฒ๐ฎ๐ฆ๐›๐š๐ง๐ข?

๐Š๐ฎ๐๐ก๐ข๐›๐ข๐ญ๐ข ๐ฉ๐ซ๐ž๐ฌ๐ก๐š: ๐‰๐ž, ๐ง๐ข ๐ฅ๐š๐ณ๐ข๐ฆ๐š ๐ง๐ข๐ฐ๐ž ๐ง๐š ๐ค๐ข๐ฉ๐ข๐ฆ๐จ ๐œ๐ก๐š ๐ฉ๐ซ๐ž๐ฌ๐ก๐š ๐ง๐ฒ๐ฎ๐ฆ๐›๐š๐ง๐ข?

Dr Adinan

Member
Joined
Jul 11, 2021
Posts
14
Reaction score
22
Presha ni ugonjwa unaosababisha vifo na ulemavu wa kudumu. Unaweza kudhibiti presha na kuepuka madhara yake kama utachukua hatua stahiki mapema. Ila....

Ubaya wa ugonjwa huu ni kwamba presha inaweza kuwa juu kiwango cha kupasua mishipa ya damu kwenye ubongo na kusababisha kiharusi au magonjwa ya figo bila kuonesha dalili hata moja.

๐Ÿ‘‰ ๐๐ฃ๐ข๐š ๐ฉ๐ž๐ค๐ž๐ž ๐ฒ๐š ๐ค๐ฎ๐Ÿ๐š๐ก๐š๐ฆ๐ฎ ๐ฎ๐ ๐จ๐ง๐ฃ๐ฐ๐š ๐ก๐ฎ๐ฎ ๐ง๐ข ๐ค๐ฎ๐ฉ๐ข๐ฆ๐š ๐ญ๐ฎ! ๐Ÿ‘†

Nimekuwa nikiulizwa swali hili mara nyiningi, ๐‰๐ž, ๐ง๐ข ๐ฅ๐š๐ณ๐ข๐ฆ๐š ๐ง๐ข๐ฐ๐ž ๐ง๐š ๐ฏ๐ข๐ฉ๐ข๐ฆ๐จ ๐ฏ๐ฒ๐š ๐ฉ๐ซ๐ž๐ฌ๐ก๐š ๐ง๐š ๐ค๐ข๐ฌ๐ฎ๐ค๐š๐ซ๐ข ๐ง๐ฒ๐ฎ๐ฆ๐›๐š๐ง๐ข?

Ingawa ni LAZIMA kupima ili kuweza kudhibiti presha na kuepuka madhara yake, si lazima kuwa na vifaa hivi nyumbani.

Hatahivyo kuna faida nyingi za muhimu za kuwa na vifaa hivi nyumbani. Nikiwa kama daktari nakushauri kuwa na vifaa hivi nyumbani. Fahamu sababu.

Sababu moja ya msingi inayozaa faida nyinginezo ni kwamba kuwa na vifaa hivi nyumbani hukuwezesaha kufahamu hali yako ya presha kwa uhakika wakati wowote ule. Kumbuka mlango wa tiba ya presha uko kwenye kufahamu kiwango cha presha.

Kama tulivyoona hapo juu, ubaya wa ugonjwa wa shinikizo la juu damu โ€“ presha ni kwamba presha inaweza kuwa juu na kuendelea kuleta madhara bila kuonesha dalili hata moja! Kufahamu hali yako ya presha kwa uhakika wakati wowote ule huja na faida zifuatazo:

1. Sasa, unaweza kutathmini tiba yako Kama unatumia dawa au njia zingine za kudhibiti shinikizo la damuโ€ฆnamna pekee ya kufahamu kama unaendele vizuri ni kupima shinikizo la damu. Fahamu na furahia kwasababu tiba unayoendelea nayo inafanya kazi. Fahamu na chukua hatua mapema kama tiba unayoendelea nayo haifanyi kazi ipasavyo. Hivyo, sasa unaweza kuchukua hatua stahiki mapema kuepuka madhara ya kisukari na presha.

2. Sasa unaweza kuchukua tahadhari kuepuka presha โ€“ Tafiti zinaonesha kwamba ukitambua hali yako mapema hatari ya kupata madhara hupungua kwasababu utachukua hatua mapema. Fahamu na chukua hatua mapema kama tiba unayoendelea nayo haifanyi kazi ipasavyo. Hivyo, sasa unaweza kuchukua hatua stahiki mapema kuepuka madhara ya kisukari na presha.

3. Ondokana na hofu unapokuwa na vifaa hivi โ€“ Kwa uzoefu wangu, mtu anapogundulika na presha hupata huzuni ghafla na kuanza kufikiria athari ambazo amekwisha kuziona zikiwatokea watu anao wafahamu. Mtu huanza kufikiri vipi nikipata shambulio la moyo au kiharusi kama fulani.

Madhara yote haya sasa unaweza kuyaepuka kwasababu sasa unaweza kuchukua hatua stahiki mapema kulingana na kiwango chako cha sukari kwa kuwa unafahamu. Faida nyenginezo ni kwamba sasa unakuwa na muda mwingi wa kupumzika na kukaa na familia yako badala ya kutumia muda huo kwenda hospitali na kukaa kwenye foleni.

Faida ingine muhimu ni kuokoa gharama za matibabu ya madhara ya presha. Madhara ya presha, mfano kiharusi, figo kufeli, yanagharimu pesa nyingi za matibabu na unashindwa kufanya shughuli zako za kungeza kipato chako kwani muda mwingi unakuwa kwenye matibabu.
 
Dah maandiko ya faida kama hili yanapita tu hivihivi ...asante Kwa elimu,ila Mimi tatizo lingine naloliona ni kuwa wengi hata hatujui ili Pressure iwe normal kipimo kisome vipi pia ikiwa abnormal iwe ngapi
Na hata hivyo vifaa vyenyewe bei si rafiki
 
Wewe ni dokta kweli? Unashindwa kutaja visababishi , hata kimoja dalili hata mojร ..au au unapiga winga kwenye udokta kama winga wa simu kariakoo
 
Back
Top Bottom