A
Anonymous
Guest
Mimi nilifanya mafunzo ya internship nikiwa kama daktari katika hospitali ya Lugalo kuanzia Nov 2021 mpaka Nov 2022. Hospital ina utaratibu wa kulipa call allowances kwa madaktari na nurses wanaokaa shift za usiku kila mwezi. Ajabu iliyoje miezi miwili ya mwisho yaani September na October 2022, kada zote mbili za madaktari na manesi hatukulipwa pesa zetu.
Viongozi wetu walifatilia, tukaambiwa tutume mpaka bank statement, tulituma na wakakiri walikosea sehemu na wangetulipa kabla ya June 2023, lakini mpaka leo kimya.
Kiongozi alifuatilia na baadae ikawa hospital management inapiga chenga haitoi majibu ya uhakika. Hii imefanya mpaka baadhi yetu kuamini kuwa pesa zetu ambazo kila mtu alikuwa akidai Tsh 400,000/= na ni zaidi ya interns 80 wanadai, zimeliwa na watendaji wa hospitali ambao sio waaminifu.
Nimeamua kuandika kwenye jukwaa hili pengine sauti yetu ikisikika kwenye mitandao ya kijamii hasa JamiiForum, tunaweza kupata haki yetu. Na hii ni baada ya kiongozi wetu kukiri kwamba amechoka kufatilia na hizo pesa hatutazipata tenaa.
Nawasilisha na kuambatanisha whatsupp chat za group letu.